PETR CECH: WALETENI HAO MANCHESTER CITY NA MANCHESTER UNITED

Dimba - - Special - LONDON, England

MLINDA mlango wa klabu ya Arsenal, Petr Cech, amesema timu yake ina ari ya kuzichapa timu zinazotesa kwa sasa Premier League, Man United na City na kufuta gepu la pointi baina yao katika nafasi za juu kwenye msimamo.

‘The Gunners’ waliinyuka Brighton mabao 2-0 wikiendi iliyopita na imeelekea katika mapumziko ya mechi za kimataifa ikiwa nafasi ya tano, pointi sita nyuma ya City na United. Wakiwa juu pia ya Liverpool ambao miezi michache iliyopita waliwanyuka 4-0 kiasi cha kuwaacha wadau wake na maswali lukuki juu ya uwezo wao wa kiushindani msimu huu.

“Bado hatujacheza na City, United, hivyo tuna fursa ya kuwasogelea zaidi,” alisema.

“Tangu tulipofungwa na Liverpool tumerudi na nguvu mpya. Kila mtu anaifanya kazi yake vizuri na kupata matokeo ambayo yanatufanya tujiamini.

“Tunacheza soka safi kama timu. Makosa yetu tunayasahihisha kwa kujituma zaidi hasa kwenye idara ya ulinzi. Tunasonga mbele,” aliongeza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.