Mashabiki wapora zawadi Moro

Dimba - - Special -

TIMU ya soka ya Black Viba imeporwa zawadi ya ubingwa wa mashindano ya kugombania jezi na timu ya Moro City.

Uporaji huo ulifanywa na mashabiki wa timu ya Moro City, baada ya kuanzisha fujo mara tu timu ya Black Viba ilipotangazwa mshindi na kukabidhiwa zawadi ya ubingwa.

Mchezo huo wa fainali ulichezwa Jumapili katika Uwanja wa Kikundi, Morogoro Mjini, ambapo timu ya Black Viba ya Viwandani ilifanikiwa kuibuka kidedea dhidi ya timu ya Moro City ya Kichangani, baada ya kupata bao kwa njia ya penalti katika dakika ya 50.

Penalti hiyo iliamriwa baada ya mchezaji wa Moro City kuunawa mpira ndani ya box, ambapo mchezaji wa Black Viba, Paty Edo, alipiga penalti iliyotikisa nyavu za timu pinzani, ushindi uliosababisha Black Viba kuibuka kidedea wa mashindano hayo na kuzawadiwa zawadi ya seti ya jezi.

Lakini baada ya mabingwa kupewa zawadi hizo, mashabiki wa timu ya Moro City walianzisha fujo na kuwapora jezi, viatu na nguo zao nyingine wachezaji wa timu ya Black Viba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.