Gairo, Sabasaba hapatoshi leo

Dimba - - Special -

TIMU ya soka ya Halmashauri ya Gairo (GDC ze Orange) inatarajia kushuka dimbani leo kuumana na timu ya Sabasaba ya Mjini Morogoro, katika michuano ya ligi daraja la tatu inayoendelea kutimua vumbi katika kituo cha Mvomero, mkoani Morogoro.

Timu hizo zote, licha ya kukabiliwa na ukata, lakini zimetambiana kuwa zimejiandaa kikamilifu kila moja kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Kocha wa timu ya GDC ze Orange, Buya Kassim, aliliambia DIMBA kuwa, kikosi chake kiko imara na ana uhakika kuwa wataibuka na ushindi katika mchezo huo.

ìKiufundi tumejipanga kikamilifu, kikosi changu hakina matatizo na kamati ya ufundi inaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha tunaibuka na ushindi katika mchezo huo kesho (leo),î alisema.

Naye Katibu Mkuu wa timu ya Sabasaba, Abubakari Mkingie, amesema wamejipanga kuhakikisha wanachukua pointi zote tatu.

ìKamati ya ufundi inaendelea kufanya kazi kadri inavyoweza ili kuhakikisha tunachukua pointi zote tatu, katika mchezo huo tumeweka pembeni shida zinazotukabili (ukata) na kujiwekea malengo ili kuhakikisha tunavuna pointi ndipo tutaendelea kuwa sawa kiuchumi,î alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.