RAFAEL NADAL

Rafael Nadal anamiliki utajiri wa dola Mil.89

Dimba - - Special - MANACOR, HISPANIA

K ATI ya majina ya nyota waliojipatia jina kubwa pamoja na kujiingizia kipato kikubwa katika mchezo wa tenisi ni Rafael "Rafa" Nadal Parera, mtoto wa Sebastián Nadal pamoja na Ana María Parera, ambaye amezaliwa kitongoji cha Manacor kilichopo Mallorca, eneo maarufu kwa mapango ya Drach.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 31, ambapo tayari amekwishatwaa mataji 16 makubwa ya mchezo wa tenisi Grand Slams na kushika nafasi ya pili nyuma ya Roger Federer mwenye mataji 19.

Mbali na mataji hayo, nyota huyo anashikilia medali mbili za dhahabu alizopata katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2008 Beijing, China na nyingine 2016, Rio de Janeiro, Brazil.

Mkali huyo pia anamiliki utajiri wa dola za Marekani milioni 89,989,600 ambazo ni sawa trilioni 199,417,000,000 za Kitanzania na kuingia katika orodha ya nyota wanaomiliki kiasi kikubwa cha fedha.

Yafuatayo ni mambo matano yanayomhusu nyota huyo ambayo yameandaliwa kwa msaada wa mitandao mbalimbali.

Nyota huyo mwenye kipaji cha aina yake katika mchezo wa tenisi, alianza kuhesabu mataji akiwa na miaka nane tu alipobeba taji la mkoa kwa vijana wenye umri wa miaka 12, ambapo ndipo safari yake ilipoanzia.

AKIWA NA MIAKA 17, ALIMWONDOA FEDERER WIMBLEDON

Nadal mwenye rekodi lukuki aliwaacha vinywa wazi pale alipofika hatua ya tatu ya mashindano ya Wimbledon akiwa na miaka 17 tu na kufanya kazi ya ziada kumwondoa mkali Roger Federer aliyekuwa katika kiwango cha hali ya juu kipindi hicho.

ALIWAHI KUBEBA MATAJI NANE MFULULIZO YA MONTE CARLO

Nadal ambaye anarekodi inayovutia ni kati ya watu wanaochungwa zaidi kutokana na uwezo wake mkubwa uliosababisha atwae mataji nane mfululizo ya mashindano ya Monte-Carlo kuanzia mwaka 2005 hadi 2012, ambapo ufalme wake ulivunjwa.

ABEBA TAJI LA FRENCH OPEN AKIWA NA MIAKA 19

Akiwa na miaka 19 tu, Nadal alibeba taji kubwa la mchezo wa tenisi la French Open ambalo limekuwa likitolewa macho na vigogo wengi wa mchezo huo duniani kote.

ANAMILIKI KITUO CHA TENISI NCHINI INDIA

Licha ya mafanikio aliyoyapata nyota huyo ana kiu ya kuona mchezo wa tenisi ukizidi kufika mbali zaidi, ndio sababu iliyosababisha afungue kituo cha mchezo huo katika kitongoji cha Anantapur, Andhra Pradesh, India ambacho amekipa jina lake Nadal Tennis School.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.