VPL mzunguko wa tano dakika 7,200, mabao 76, pointi 105

Dimba - - Special - NA MARTIN MAZUGWA katika mchezo hata mmoja katika mechi tano walizoshuka uwanjani.

LIGI Kuu ya Tanzania Bara imeendelea kushika kasi kwa klabu tatu kuchuana kuwania kushika uongozi katika msimamo ambao kinara ni wekundu wa Msimbazi, Simba, wenye alama 11, sawa na Azam FC pamoja na Mtibwa Sugar, wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Simba ndiyo klabu pekee hadi sasa yenye idadi kubwa ya mabao ya kufunga mara baada ya mechi tano kwa kupachika mabao 14, ambayo hayajafikiwa na timu yoyote.

Wekundu hao wa Msimbazi wamevunja rekodi ya Yanga ya msimu uliopita ambapo katika michezo mitano vijana hao wa Jangwani walikuwa wamepachika mabao 12.

Msimu huu umekuwa na presha kubwa, hasa kwa vijana wa Jangwani ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu, kwani katika michezo mitano waliyoshuka uwanjani wamepachika mabao manne pekee, huku wakijikusanyia pointi tisa na kushika nafasi ya tano. YANGA YAFUNGA MABAO MACHACHE ZAIDI KATIKA MECHI TANO ZA AWALI NDANI YA MISIMU SITA

Huenda huu ukawa ndio msimu pekee ambao Yanga wamefunga mabao machache zaidi katika kipindi cha misimu sita ya hivi karibuni katika michezo mitano ya awali.

Tangu msimu wa 2012/13 Yanga haikuwahi kufunga mabao chini ya matano katika michezo mitano ya awali, ambapo rekodi inaonyesha msimu wa 2012/13 ilifunga mabao saba, 2013/14 ikafunga kumi, huku 2014/15 ikifunga saba.

Msimu wa 2015/16 ikafunga 13 na mwaka uliopita ikifunga mabao 12, huku msimu huu ikiwa na mabao manne pekee.

ABAROLA MLINDA MLANGO PEKEE ALIYERUHUSU BAO MOJA

Moja kati ya walinda mlango walioonyesha kiwango cha kushangaza msimu huu ni kipa mpya wa klabu ya Azam FC raia wa Ghana aliyesajiliwa msimu huu kuziba nafasi ya Aishi Manula, aliyetimkia katika klabu ya Simba.

Nyota huyo ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kuwa mlinda mlango pekee aliyeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja pekee mara baada ya michezo mitano.

WAGENI WAWATOA JASHO WENYEJI

Msimu huu umekuwa wa kuvutia kwa klabu zilizopanda daraja, licha ya ugeni wao zimedhihirisha kuwa hazikupanda Ligi Kuu kimakosa. Singida United wanashika nafasi ya nne, huku Lipuli ikikamata nafasi ya 10 na Njombe mji ikishika nafasi ya 11.

KAGERA SUGAR WATIA FORA

Licha ya kufanya usajili kwa kuziba nafasi zilizokuwa na mapungufu mwaka uliopita, timu hiyo iliyoshika nafasi ya tatu msimu uliopita imeshindwa kufanya lolote la maana na kujikuta ikiburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania, mara baada ya kushuka dimbani katika michezo mitano.

Mwaka huu ni msimu pekee ambao wakatamiwa hao wameshindwa kuibuka na ushindi NYOTA WA KIGENI WAANZA NA MOTO VPL

Wachezaji wa kigeni wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara baadhi yao wameanza kufungua akaunti zao za mabao, huku kinara wa ufungaji akiwa ni mshambuliaji raia wa Uganda, Emanuel Okwi, ambaye hadi sasa ana mabao sita katika michezo minne aliyoshuka uwanjani.

Nyota wengine walioanza kuwasha moto ni mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma, Michelle Katsvairo wa Singida United, ambao kila mmoja amepachika mabao mawili.

Wengine ni Dany Usengimana wa Singida United, Laudit Mavugo wa Simba pamoja na raia wa Ghana, Yahaya Mohamed wa Azam FC, ambao hao wote kila mmoja amefunga bao moja.

MWADUI, RUVU SHOOTING ZAONGOZA KWA KUFUNGWA MABAO MENGI

Hadi mzunguko wa tano unakamilika ni timu mbili pekee zimeruhusu wavu wao kutikiswa mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote, ambayo ni matajiri wa madini, Mwadui na maafande wa Ruvu Shooting, ambao kila mmoja ameruhusu mabao kumi katika michezo mitano.

Msimu uliopita timu iliyokuwa imeruhusu mabao mengi katika mechi tano za awali ilikuwa JKT Ruvu, ambayo iliruhusu wavu wake kuguswa mara 12.

Wachezaji wa Yanga

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.