Ukata waikata Mzuka GDC Gairo

Dimba - - Special -

TIMU ya soka ya Halmashauri ya Gairo (GDC ze Orange) ambayo inacheza Ligi Daraja la Tatu, ipo kwenye hatihati ya kuendelea kucheza ligi hiyo kutokana na kukabiliwa na ukata mkali.

Nahodha wa timu hiyo, Romani Ngarunda, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa timu hiyo inakabiliwa na hatari ya kushindwa kuÀka uwanjani kutokana na kukosa nauli, chakula na mahitaji mengine muhimu.

“Mfano ni mchezo wa leo (jana) dhidi ya timu ya Geto ya Mvomero, mpaka sasa hatujajua kama tutaweza kusaÀri kutoka Gairo kwenda Mvomero kucheza mechi hiyo, maana mfukoni tuna shilingi 35,000 wakati usaÀri pekee ni shilingi 100,000 bado wachezaji hawajala, wadau wameitunyima ushirikiano kabisa,” alisema.

Timu hiyo ambayo imepangwa katika kituo cha Mvomero ilikuwa inahitaji sare au ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya timu wenyeji ya Geto ili iweze kusonga hatua ya pili.

Katika mchezo wake wa kwanza ilifungwa na timu ya Sabasaba ya Morogoro Mjini kwa 4-2 lakini ilizinduka katika mchezo wa pili dhidi ya Obtala ya Mvumero ambapo ilishinda kwa bao 4-0.

Wakati huo Meneja wa timu hiyo, Shaban Mumbi, amesema yuko nje ya Mkoa wa Morogoro kikazi ila anahangaika kadiri atavyoweza kuona kama ataweza kuisaidia timu japokuwa ameomba wadau wa soka wa Gairo kumuunga mkono, kwani hiyo timu inawakilisha Wilaya ya Gairo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.