Nusu fainali Rwakatare Ndondo Cup Okt 23

Dimba - - Special -

KAMATI ya mashindano ya soka ya Rwakatale Ndondo Cup imetangaza kuwa hatua ya nusu fainali itaanza Oktoba 23 mwaka huu katika bonde la Mngeta, Uwanja wa Lukolongo wilayani Kilombero, mkoani Morogoro.

Mratibu wa mashindano hayo, Superatus Duma, ameliambia DIMBA kuwa hatua hiyo itachezwa kwa siku mfululizo ambapo timu ya Serengeti FC na Shupavu FC zinatarajia kufungua dimba hatua hiyo.

Duma alisema mchezo utakaofuata utakuwa kati ya timu ya Toto FC dhidi ya Mlambani FC, JKT Chita vs Wales, Mahakama vs Mngeta, Mnagers vs Kijiwe, Express vs Mwaya B, Street FC vs City Boys na Mlimba City vs Idete FC.

“Baada ya hapo zitabakia timu nane na tutazigawanya katika makundi mawili ambapo zitacheza katika mfumo wa ligi ili kupata timu mbili zitakazocheza hatua ya fainali ya mashindano hayo,” alisema.

Mashindano hayo ambayo awali yalichezwa katika vituo sita kwa kujumuisha wilaya zote za Kilombero, yaliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare, ambaye ni mzaliwa wa Mngeta wilayani Kilombero, mkoani Morogoro.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.