Mo Dewji aanza na uwanja Simba

Dimba - - Mbele - NA SAADA SALIM

SIMBA hii ya kimataifa. Hivi ndivyo unavyoweza kuizungumzia klabu hiyo, baada ya uongozi wake kusema kazi ya kwanza atakayokuwa nayo mwekezaji wao ni kushughulikia Uwanja wao wa Bunju.

Kwa sasa Simba wameshatangaza kwamba anayehisi anaweza kuweka hisa ya 50%, yenye dhamani ya Sh bilioni 20, anakaribishwa, kitu ambacho kinampa nafasi Mohamed Dewji 'Mo,' ambaye ndiye aliyeonyesa nia hiyo tangu mwanzo.

Kamati ya utendaji ya klabu hiyo imeamua kuachana na suala la uwanja kwa sasa hadi hapo mchakato wa kupatikana kwa mwekezaji utakapokamilika, huku asilimia kubwa akitajwa bilionea, Mohammed Dewji (MO), ambaye kwa sasa ni mlezi wa timu hiyo.

Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe, ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, shughuli za ujezi wa uwanja wao uliopo Bunju, zimesimama kwa muda kupisha mchakati huo na utakapokamilika mambo yataendelea kama kawaida.

"Kwa sasa viongozi tumekuwa makini katika suala la kusimamia timu yetu na maendeleo ya klabu, huku suala la uwanja tukisubiri, kwani tunahitaji utengenezwe wa kisasa zaidi, ikiwamo hosteli za kukaa wachezaji wetu inapoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi," alisema.

Kashembe alisema pia katika ujenzi huo wa uwanja kutapatikana kila mahitaji yote yanayohitajika kwa wachezaji wao, ikiwamo sehemu ya kuogelea na mazoezi ya viungo (gym).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.