Yanga waifuata kibabe Kagera Sugar

Dimba - - Jumatano - NA CLARA ALPHONCE

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuondoka leo kwenda Bukoba kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar, utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Yanga wanaondoka wakiwa kamili kwa ajili ya mchezo huo wakiwa na hasira ya kulazimishwa sare na Mtibwa Sugar wiki iliyopita.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alisema timu hiyo itaondoka na basi kwenda Bukoba na baada ya michezo yake hiyo miwili wataendelea kusalia Mwanza kwa ajili ya kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.

Alisema kwa ujumla maandalizi yote ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar na Stand United yapo vizuri na wanatarajia kufanya vizuri katika michezo huo, ili iwe chachu ya kuwafunga Simba.

Naye Kocha Msaidizi, Shadrack Nsajigwa, aliwataka mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho timu yao haifanyi vizuri, kwani muda si mrefu watarudi katika kiwango chao.

Alisema kubwa ambalo lilikuwa linawasumbua katika timu yao, ni majeruhi kwa baadhi ya wachezaji lakini wanashukuru wameanza kurejea na baada ya kucheza mechi kadhaa watarudi katika ubora wao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.