Njombe Mji, Lipuli, hatumwi mtoto dukani

Dimba - - Jumatano - NA MAREGES NYAMAKA

WAKATI idadi kubwa ya mashabiki ikingojea kwa hamu kubwa michezo ya timu kongwe za Simba na Yanga zitakapokuwa kibaruani mwishoni mwa wiki hii, mashabiki hao wanasahau kuwa mchezo kati ya Njombe Mji dhidi ya Lipuli FC si wa kukosa.

Timu hizo ambazo ni majirani zinatarajiwa kukutana Jumamosi ya wiki hii, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Samora, ambapo ukiachana na mchezo kati ya Simba watakaowakaribisha Mtibwa Sugar na Yanga watakaokuwa wageni wa Kagera Sugar, huu nao ni mchezo mgumu.

Wawili hao wanatoka Nyanda za Juu Kusini ambapo zote ndio zimepanda daraja msimu huu kitu ambacho kitaufanya mchezo huo kuwa mkali kila moja ikitaka matokeo mazuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.