Mashabiki wachangia ujenzi Uwanja wa Kaunda

Dimba - - Jumatano - NA CLARA ALPHONCE

MASHABIKI wa klabu ya Yanga wameanza kuchangishana fedha kwa ajilli ya kukarabati Uwanja wa Kaunda ambao watakuwa wanautumia kwa ajili ya mazoezi msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tayari uongozi umeanza mchakato huo kwa kujaza kifusi cha mchanga katika uwanja huo.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alisema wanachama wa Yanga kwa umoja wao wameamua kusaidia ujenzi wa uwanja huo, kwa kuchangishana fedha ambazo kwa sasa zinasaidia kujaza mchanga.

“Kumekuwa na mwamko kutoka kwa mashabiki ambao wamekuwa wakichangishana kwenye makundi ya kwenye mitandao ya kijamii, watu binafsi ambao kwa dhati wanataka kuona Yanga inapiga hatua.

“Moja kwa moja siwezi kuweka wazi ni kiasi gani cha fedha ambacho tumepata mpaka sasa, kwa sababu kila tukipata tunaingiza moja kwa moja kwenye shughuli za uwanja,” alisema Ten.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.