StarMedia yakusanya washiriki 700

Dimba - - Jumatano - NA MWANDISHI WETU

JUMLA ya washiriki 700 wanatarajia kuonyesha kazi katika usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuingiza Sauti katika tamthiliya na filamu za kigeni zoezi ambalo litafanyika Jumamosi hii katika Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Huu ni msimu wa pili wa shindano hilo linaloratibiwa na Kampuni ya Star Media(T) kupitia nembo ya StarTimes ambapo washindi 10 walipatikana na tayari saba kati yao wapo nchini China wakifanya kazi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko,Star Media (T) Ltd,Li Kun, washiriki ambao wamekwishajiandikisha hadi sasa ni zaidi ya 700 na wanategemea wengine zaidi kwa muda uliobaki.

Awali zoezi hilo la usaiili lilifanyika jijini Mwanza ambapo mamia ya washiriki wanaume, wanawake na walemavu pia walifika kuonesha umahiri wao katika kuingiza Sauti ambapo sasa ni zamu ya Dar es Salaam.

Miongoni mwa washiriki hao ni msanii wa Muziki wa kizazi kipya ìPipiî. Pipi alionyesha uwezo mkubwa wa kuingiza sauti na hivyo kupata nafasi ya kuingia fainali ya Shindano hilo jijini Dar es Salaam mwisho wa mwezi huu.

Msanii wa maigizo, Nyamayao ni miongoni mwa washindi wa mwaka jana na tayari ameshatua nchini kwa ajili ya kutioa hamasa kwa watanzania kushiriki katika shindano hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.