MIAKA MIWILI YA JURGEN KLOPP, LIVERPOOL

Dimba - - Special - MERSEYSIDE, LIVERPOOL

WIKIENDI hii Jurgen Klopp atawaongoza vijana wake kuivaa Man United nyumbani kwenye mchezo wa Premier League, ikiwa ni wiki ya kusherehekea miaka miwili ya kuwapo Liver.

Kocha huyo ameiwezesha timu hiyo kutinga fainali mbili kubwa za makombe sambamba na kumaliza msimu ndani ya ‘top four’, lakini kumekuwa na malalamiko juu yake kutokana na kiwango cha sasa cha vijana wake.

Hapa tumekuandalia tathmini ya wachezaji 12 aliowasajili akiwa Liver na kuangalia nani aliyembeba na nani ambaye amemwangusha baada ya kumsajili.

STEVEN CAULKER

Ndiyo, Klopp alimchukua kwa mkopo beki huyo kutoka QPR na kumtumia kwenye mechi tano tu, lakini kiufupi Caulker alichemsha na kumweka Klopp kwenye kikaango cha mashabiki.

Caulker hakuwa na msaada wowote kwa Liver, na kwa kuwa kupata nafasi kwake ilikuwa ni ndoto, kuna siku Klopp aliwahi kumuinua benchi na kumwambia akacheze straika!

MARKO GRUJIC

Kinda huyo mwenye kipaji, alisajiliwa mwaka 2016, lakini hakutua rasmi Liver na kuachwa Red Star Belgrade, ambako alicheza kwa mkopo.

Tangu aje Liver, Grujic amecheza mechi 11, lakini hakuna kitu alichokifanya cha faida kwa Liver, iwe Ligi Kuu au michuano mingine muhimu na hata nafasi yake kikosi cha kwanza si ya uhakika wa asilimia 90.

SADIO MANE

Jembe hilo. Mane alitua Anfield kwa kitita kinono cha pauni milioni 36, akitokea Southampton, na hadi sasa ameichezea Liver mechi 37 na kufunga mabao 16. Kiwango chake kimeizidi mno fedha iliyotumika kumnunua na kumweka Klopp kwenye wakati mgumu wa kushindwa kuelewa kwanini alikuwa analaumiwa kwa kufuja fedha zote hizo kwa mtu kama Mane.

Mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Arsenal, Mane alikuwa hakamatiki kwa kupiga bonge la bao na tangu hapo amekuwa na uwiano mzuri wa kufunga mabao Ligi Kuu kulingana na mashuti aliyojaribu (30%) na licha ya kukosa mechi nyingi za mwisho msimu uliopita, bado alijumuishwa kwenye kikosi bora cha msimu 2016-17.

GEORGINIO WIJNALDUM

Mholanzi huyo amefanya vizuri kwa kiasi chake tangu atue Liver kwa dau la pauni milioni 25, akitimka kutoka Newcastle United, ambapo mechi 53 alizocheza ameweza kufunga mabao sita muhimu mno.

Ingekuwaje kama Wijnaldum angechezeshwa eneo la ushambuliaji kama alivyokuwa Newcastle na kufunga mabao 11? Kitendo cha Klopp kumtumia kama box to box midfielder kimepelekea makali yake kupungua na ndiyo maana mashabiki wa Liver bado wanaamini Wijnaldum ana vitu vingi vya kuonesha zaidi ya mabao yake dhidi ya Man City, Arsenal na Middlesbrough.

LORIS KARIUS

Hapa Liver inabidi iwe na subira sana kama ilitegemea kumuona Karius akiwa kipa namba moja ndani ya miaka michache ya hivi karibuni. Kiufupi, waendelee kuburudika na huduma ya Simon Mignolet.

Karius amekuwa mhanga wa makosa ya kizembe akiwa langoni, licha ya kuaminiwa sana Klopp, ambaye alimpa nafasiwenye mechi dhidi ya Arsenal na Seilla msimu huu.

JOEL MATIP

Hivi karibuni Matipamekuwa akipondwa kutokana na bao waliloewcastle fungwa Liver dhidi ya Newcastle wikiendi iliyopita, ila kwa mtu kama yeye na hadhi ya Liver livyo kwa sasa, ni bonge la beki.

Matip alinaswa kwa uhamisho wa bure kutoka Schalke 0na amemoja fanikiwa kufunga baokatika mechi 37, huku msimuwake wa kwanza ndio uliokuwa bora, akioka nesha uwezo wake katikuumiliki mpira na kucheza vizu i mipira ya juu kutokana na urefu wake, ingawa msimu huu, inaonekan a presha imemzidi.

RAGNAR KLAVAN

Babu huyo alitua Anfield akitokea Augsburg kwa dau la pauni milioni 4.2 na katika mechi 28 alizocheza, ana bao moja, lengo kubwa la kusajiliwa kwake ni uzefu wake na soka la Ulaya, lakinikupata nafasi imekuwa ndoto kwake, kwani amekuwa si mwepesi va kuonesha makali yake dhidi ya timu kubwa kama anavyofanya akiheza dhidi ya vibonde.

MOHAMED SALAH

Winga huyo amekuja na moto sana mwaka huu, akitokea AS Roma, baada ya Liver kulipa dau la pauni 34.3 ili kupata huduma yake, na katika mechi 11 alizocheza amefanikiwa kucheka na nyavu mara sita. Tunaweza kusema maisha yake ndani ya Liver ni kama ya Mane, kutokana na fedha zilizotumika kumchukua.

Wanaoshindwa kumwelewa ni wachache, na wale wanaomkubali kwa kasi, mabao yake ni wengi, kwani amekuwa mtu muhimu katika mfumo wa mashambulizi makali wa Klopp, akiwa sambamba na akina Phillipe Coutinho, Mane na Roberto Firmino.

ANDREW ROBERTSON

Robertson alitua Liver akitoka Hull City mwaka huu kwa dau la uhamisho la pauni milioni 10, akicheza mechi mbili ambazo zimedhihirisha sasa Liver imeondoa nuksi ya kupata mabeki wa kushoto wa hovyo tangu John Arne Riise aondoke.

Msokitishi huyo kila alipopewa nafasi ya kuonesha cheche zake, hakufanya makosa na kwa kiasi kikubwa amemfanya hata Alberto Moreno kunoa kiwango chake, hasa akijua vita iliyo mbele yake si ya kitoto.

DOMINIC SOLANKE

Licha ya kwamba kinda huyo wa zamani wa Chelsea hajafanikiwa kufunga bao lolote la mechi za kiushindani, lakini kitendo tu cha kuaminiwa na Klopp na kucheza mechi nne akitokea benchi, kinamaanisha Solanke ni mchezaji ambaye siku yoyote ana uwezo wa kupata namba kikosi cha kwanza na asipate mpinzani.

ALEX OXLADECHAMBERLAIN

Klopp aliamua kuchota pauni milioni 35 kutoka kwenye bajeti yake ya usajili na kumbeba winga huyo kutoka Arsenal ambaye hadi sasa ameonekana dimbani mara sita, ila haridhishi.

Hata hivyo, ni mapema sana kuanza kuhoji kiwango chake, kwani hata Liver kwa ujumla haipo sawa, ambapo tangu Chamberlain ametua Anfield, timu yake imeshinda mechi moja tu dhidi ya Leicester.

Ingawa amekuwa akijaribu kutimiza kila jukumu ambalo Klopp anataka litimizwe, tusubiri kuona atacheza nafasi gani na kwa muda upi, ikizingatiwa Naby Keita anatarajiwa kutua Anfield mwakani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.