NYOTA ZETU

Dimba - - Special - Utabiri huu unaletwa kwenu na Mnajimu mashuhuri Tanzania, Ramadhani Yahya, anapatikana Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam au Hale, mkoani Tanga, simu namba 0655 545462

MIZANI (LIBRA) SEPT 24 - OKT 23

Jambo fulani la muhimu kwako litasimama na kukukatisha tamaa, lakini ipo njia nyingine ya kuweza kufanya mambo yako bila kukwama, chakubadilisha ni tabia yako ya dharau na kuwa na hasira katika mambo madogo.

NGE (SCROPION) SEPTEMBA 24-OKTOBA 22

Unatesa mioyo ya wenzako kutokana na kutoelewa mambo kirahisi, una damu ya kupendwa mno mpaka inakuwa kero. Rudisha imani yako nyuma umhurumie yule unayemtesa. Ni wakati mzuri wa kupata riziki usiyoitarajia.

MSHALE (SAGITARIUS) NOV 23-DES 21

Baada ya kuhangaika sana una siku chache mno za kuitikiwa kilio chako, chagua mambo muhimu katika maisha ili uyafanyie kazi mapema.

MBUZI DESEMBA 22-JANUARI 20

Uhusiano wenu wa kimapenzi upo mikononi mwako wewe unaweza kuuendeleza au kuuzima, mwenzako hana lolote zaidi ya kusikiliza utakalo wewe.

MASHUKE (VIRGO) AGO 24 - SEPT 23

Ndoo Januari 21-Februari 19 Utakumbana na adui atakeyetaka kutumia jina lako kwa faida yake, usipomwangalia atakuharibia mipango mingi hasa ya maisha ya kazini au familia kuwa mwangalifu.

NDOO JANUARI 21-FEBRUARI 19

Utakumbana na adui atakeyetaka kutumia jina lako kwa faida yake, usipomwangalia atakuharibia mipango mingi hasa ya maisha ya kazini au familia kuwa mwangalifu.

SAMAKI FEBRUARI 20-MACHI 20

Maneno mengi yanakufanya ukose uaminifu wa kutosha, unayo nafasi ya kuomba msaada na utasaidiwa, ila epuka hasara usijaribu kufanya biashara usiyokuwa na uhakika nayo.

PUNDA MACHI 21-APRIL 20

Amka asubuhi wiki hii na ufanye maombi ili baraka zako ziwe na uhakika, kumbuka pia sadaka na kufanya ibada itakuongezea nuru ya maisha ya dunia.

NG'OMBE APRIL 21-MEI 21

Kwanini usumbuke kiasi hiki? Bahati ya pesa unayo, nuru ya kupendwa na wengi pia unayo, tatizo lako ni kutojiamini, chukua maamuzi sasa hutajutia. Mapacha Mei 22- Juni 21 Amini kwamba yule umpendaye ana dhamira ya dhati ya

MAPACHA (GEMINI) MEI 22 - JUNI 21

Vishawishi vya kufanya jambo fulani vitakukabili wiki hii, unaweza kuzama katika mahusiano au kushiriki kupata kitu kinyume na haki yako, uwe makini nyota hii yaonyesha kufuatwa na matukio ya kuadhika na majuto.

KAA JUNI 22-JULAI 23

Kaa na u¿kiri upya juu ya maamuzi yako, usikurupuke kwa lolote hasa kati ya siku hizi 10 kuanzia siku ya nne ya mwezi ujao. Tegemea kupata hasara usipoangalia haya.

SIMBA JULAI 24-AGOSTI 23

Utapata kazi ya kuchangisha michango itakupa muda mgumu na unaweza kugombana na watu, hali yako kiafya itazidi kuimarika na masuala ya kipato chako yatasimama, mapenzi nayo yataadimika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.