JUMA MAHADHI

Sina mvuto, ndio maana mademu hawanipendi

Dimba - - Special - NA CLARA ALPHONCE

WINGA Juma Mahadh ni moja ya wachezaji waliosajiliwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga msimu wa 2016/17 akitokea katika timu ya Coastal Union ambayo imeshuka daraja.

Yanga walishawishika kumsajili mchezaji huyo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na timu yake ya Coastal Union.

Hata hivyo, mchezaji huyo mpaka sasa ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha kocha Mzambia George Lwandamina, hivyo anahitaji kufanya kazi ya ziada ili aweze kumshawishi kocha huyo.

Hata hivyo, DIMBA liliamua kumtafuta winga huyo ili watu waweze kumjua zaidi hasa katika maisha yake ya nje ya uwanja.

DIMBA: Unajulikana sana kutokana na umahiri wako katika soka, katika maisha ya kawaida wewe ni nani?

MAHADHI: Naishi maisha ya kawaida, siishi kama staa, najichanganya na watu kama kawaida, napanda daladala ama bodaboda kama watu wa kawaida tu.

DIMBA: Unaishi na nani na wapi? MAHADHI: Naishi Tabata na raÀki yangu. DIMBA: Unapenda kula chakula gani? MAHADHI: Napenda kula wali samaki. DIMBA: Unajua kupika chakula chochote? MAHADHI: Najua baadhi si vyote. DIMBA: Tofauti na kupika kazi gani nyingine za nyumbani ambazo unaweza kufanya?

MAHADHI: Ndio naweza kuosha vyombo, kufanya usaÀ ndani kwangu na kufua.

DIMBA: Unapenda kula tunda gani na kinywaji gani?

MAHADHI: Napenda kula machungwa na kinywaji ni juisi ya embe.

DIMBA: Mtindo gani wa nywele ambao unapenda kunyoa na mavazi gani ambayo unapenda kuvaa pamoja na rangi zake?

MAHADHI: Napenda kunyoa panki au afro, mavazi ninayopenda kuvaa ni pensi na T-shirt na mara chache navaa suruali na rangi ninayopenda ni nyeusi.

DIMBA: MaraÀki zako wa karibu ni watu wa aina gani?

MAHADHI: Dah… huwezi amini mi' huwa sina maraÀki kabisa na raÀki mmoja tu ndio mara nyingi nakuwa naye na asipokuwepo huwa nakuwa peke yangu tu.

DIMBA: Unakipaji gani kingine tofauti na soka? MAHADHI: Sina. DIMBA: Kama usingekuwa mcheza soka ungefanya kazi gani? MAHADHI: Fundi magari. DIMBA: Ili uwe na hasira mtu akifanyie nini na ili uwe na furaha ufanyiwe kitu gani?

MAHADHI: Mtu akiniongelea uongo na ili nifurahi mtu aniambie ukweli hata kama nikiwa nimekosea moyo wangu unakuwa na amani sana.

DIMBA: Unapokuwa na mama yako mambo gani huwa anapenda kuzungumza na wewe?

MAHADHI: Mengi ila kubwa ni kuhusu kazi yangu, wananiambia niipende kazi, changamoto ninazokutana nazo ni sehemu ya maisha zisiwe sababu ya kunikwamisha katika kazi.

DIMBA: Siku yako haiwezi kuisha bila kufanya nini?

MAHADHI: Siku yangu haiwezi kuisha bila kuongea na mama yangu pamoja na kucheza gemu.

DIMBA: Siku zote umaarufu haukosi changamoto, wewe unakutana na changamoto gani mtaani kwako?

MAHADHI: Changamoto ambayo inaniumiza sana mtaani ni pale watu wanaponiona kama mimi ni mtu wa starehe na kuanza kuniongelea vibaya, inaniumiza sana, natamani siku nije nifanye kitu kikubwa ili niweze kufuta sifa hiyo ninanyopewa.

DIMBA: Kitu gani huwezi kukisahau kwenye maisha ya soka?

MAHADHI: Siku niliyokosa penalti katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, ambapo Simba walitoka na ushindi wa penalti 5-4.

Niliumia sana maana sikutarajia kukosa nilijua watu wananilaumu sana si unajua mechi zenyewe zile za lawama.

DIMBA: Mastaa wengi wanakutana na changamoto za kusumbuliwa na wanawake au watoto wa kike, wewe unajiepusha vipi na changamoto za wanawake?

MAHADHI: Mimi sijawahi kukutana na changamoto hiyo, labda kwa sababu sina mvuto au kwa jinsi ninavyojiweka wanaogopa kunifuata.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.