EDSON ARANTES DO NASCIMENTO 'PELE'

Rekodi yake ya mabao 1,363 haijavunjwa

Dimba - - Special - MINAS GERAIS, BRAZIL

U NAPOTAJA majina ya majimbo makubwa zaidi nchini Brazil, huwezi kulikosa jina la Minas Gerais, ambalo ni la nne kwa ukubwa katika nchi ya Brazil, likiwa na mita za mraba 586,522.1, ndiyo ardhi aliyozaliwa mchawi wa soka, Edson Arantes do Nascimento ëPeleí.

Pele, aliyezaliwa Oktoba 23, 1940, ni nyota wa zamani wa Santos, New York Cosmos pamoja na timu ya Taifa ya Brazil, hivi sasa akiwa na umri wa miaka 76, ambaye kabla ya kuwa staa alikulia maisha ya dhiki katika mji wa Bauru, katika Jimbo la Sao Paulo.

Soka liligeuka kuwa mkombozi wake mara baada ya kusajiliwa na wakali Santos, ambayo ni klabu iliyowatoa nyota wengi duniani, akiwamo mchezaji ghali duniani kwa sasa, Neymar Jr.

Kutokana na uwezo wake wa soka, jina la nyota huyo limekuwa likiimbwa ulimwenguni kote kutokana na ubora aliouonyesha alipokuwa akisakata kabumbu.

Zifuatazo ni dondoo tano zinazomhusu nyota huyo wa kimataifa wa Brazil.

NI BABA WA WATOTO SITA

Katika maisha yake binafsi ya nje ya soka, Pele, nyota anayeheshimika nchini Brazil kutokana na mchango wake katika kukuza mchezo wa soka nchini humo, amejaaliwa kupata watoto sita ambao hakuna ambaye ameweza kuvaa vyema viatu vyake.

Wanawe ni pamoja na Sandra Machado, Kelly Cristina, Fl·via Kurtz, Edinho, Joshua pamoja na Celeste.

Ni mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 1363.

Ni nyota ambaye inasemekana kuwa ndiye mwanasoka wa kwanza kufikisha idadi ya mabao mengi zaidi katika mchezo wa soka kwa kupachika jumla ya mabao 1363 katika michezo 1281 aliyoshuka dimbani.

Nyota mwingine ambaye anaingia katika orodha ya watu waliofikisha zaidi ya mabao hayo ni Romario, ambaye alikuwa akimfuatia kwa karibu mkali huyo.

NDIYE MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE TIMU YA TAIFA

Washambuliaji wengi na wakali wamepita katika kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil, kama vile Romario, Rivaldo, Ronaldo de Lima, Luis Fabiano, Fred na wengine, lakini rekodi aliyoiacha Pele imeendelea kudumu hadi leo.

Nyota huyo, ambaye ameacha rekodi ya kupachika mabao 95 katika michezo 77, inaendelea kudumu, licha ya Taifa hilo kuwa na vijana wengi wenye vipaji.

ANA JUMLA YA HATTRICK 92

Katika maisha yake ya kucheza soka, Pele aliacha rekodi nyingi za kusisimua, moja ikiwa ni hat-trick nyingi zaidi kufungwa katika maisha ya soka, kwani hadi anastaafu alikuwa tayari amejikusanyia mipira 92.

Alifunga hat trick ya kwanza akiwa na miaka 17 tu. Mfumania nyavu huyo ameacha alama nyingine katika mchezo wa soka, hasa la kimataifa, kwa kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja.

Pele alifanya hivyo katika fainali za kombe la dunia mwaka 1958, katika mchezo kati ya Brazil dhidi ya Ufaransa, ambapo alifunga akiwa na miaka 17 na siku

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.