Mayanga itazame Serengeti Boys kwa upekee

Dimba - - Special -

T IMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imekuwa ikibadilishwa kila wakati kulingana na mahitaji na nyakati. Huu umekuwa ni mfumo wa timu nyingi duniani ingawa kwa Tanzania imekuwa ni tofauti kidogo kutokana na namna mfumo wa uhitaji au uchaguzi wa timu zetu ulivyo.

Kimsingi kuna mazingira ambayo wakati mwingine yanakuwa si rafiki kwa timu za Taifa, kutokana na namna soka letu lilivyo kuanzia kwenye klabu hadi timu ya taifa. Mfumo wa soka letu ambao tumekuwa tukiutumia miaka mingi umekuwa chanzo cha matatizo kwenye timu za taifa.

Wapo wachezaji ambao wamekuwa hawana ubora unastahili kuwepo kwenye timu za taifa, lakini wamekuwa wakiitwa kutokana na namna ligi zetu zilivyo ambazo kimsingi zimekuwa ni tatizo kwa kuwa hazina ubora unaostahili.

Kwa mfano, kwenye kikosi cha Stars cha sasa ambacho kimekuwa kikipewa majukumu kwa ajili ya taifa, kimekuwa na changamoto nyingi na matatizo mengi katika uendeshwaji wake.

Nilitegemea kwamba katika hali ya kawaida kabisa, kikosi cha Stars ambacho kina majukumu ya kucheza mechi za kitaifa, kingeweza kujumuisha wachezaji vijana hasa wale waliotoka katika kikosi cha timu ya taifa ya Vijana chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, kilichoshiriki michuano ya Afcon nchini Gabon mwaka huu.

Ninachokiamini mimi ni kitu kimoja kwamba, soka huwa linakwenda na linachezwa kulingana na wakati, ambapo kwa vijana waliowakilisha nchi kwenye fainali za Afcon mwaka huu ilikuwa ni moja ya kitalu cha kwanzia katika kuipa makali Stars.

Hili ndilo lingekuwa jambo kubwa katika kutekeleza maendeleo ya soka kwa sababu vijana wale wa Serengeti wangefaa waanze kupewa majukumu makubwa zaidi ili kuwa msaada mkubwa kwa siku zijazo katika nchi hii.

Ieleweke kwamba sipingi kuwepo kwa wachezaji wakubwa kwenye kikosi cha Stars, lakini inafaa kuwepo na mchanganyiko japo kwa kiwango kidogo ili kuisadia timu kwa sku zijazo.

Kwa maana hiyo sasa, Kocha wa Stars, Salum Mayanga, anaweza kuchukua maamuzi ya kuongeza baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho kwa siku zijazo kwa kuwa huo ndio utakaokuwa mwanzo wa Stars imara zaidi kwa maslahi ya nchi kwa sababu ni jambo linalowezekana.

Hakika jambo hili hakuna lisilowezekana hivyo Mayanga na wasaidizi wake wanatakiwa kuchukua hatua na maamuzi sahihi ambayo yanaweza kuisadia nchi iweze kupiga hatua katika mechi nyingine za mashindano na kirafiki kwa sababu inawezekana.

Kila la kheri Tanzania, kila la kheri Stars katika michuano ijayo ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.

Kimsingi kuna mazingira ambayo wakati mwingine yanakuwa si rafiki kwa timu za Taifa, kutokana na namna soka letu lilivyo kuanzia kwenye klabu hadi timu ya taifa. Mfumo wa soka letu ambao tumekuwa tukiutumia miaka mingi umekuwa chanzo cha matatizo kwenye timu za taifa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.