Zanzibar yaitumbulia macho ‘Budokan Cup’

Dimba - - Jumatano - NA SHARIFA MMASI

TIMU ya taifa ya mchezo wa judo upande wa Zanzibar, imeanza maandalizi kuelekea mashindano ya Kombe la Budokan ‘Budokan Cup’, yanayotarajiwa kutimua vumbi Desemba 16, mwaka huu, mjini Unguja. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Chama cha Judo Zanzibar (ZJA), Muhammed Khamis, wachezaji watakaoshiriki mashindano hayo kwa uzito tofauti wameanza kujifua ili kujiweka sawa. “Kwa sasa hatuna mashindano yoyote mbele yetu hadi hapo Desemba mwaka huu, hivyo wachezaji wote wanaendelea na mazoezi ya mmoja mmoja kuelekea kwenye kivumbi hicho,” alisema. Muhammed alisema mashindano hayo yatashirikisha wachezaji kutoka pande mbili za Muungano wa Tanzania huku wanaume wakipigania uzito wa kg 60, 66,81 na zaidi huku wanawake ukianzia kg 48,52,57 na kuendelea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.