Wanne wavu kuwakilisha Tz Kimataifa

Dimba - - Maoni - NA ZAINAB IDDY

WACHEZAJI wanne wa mchezo wa wavu, wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya mchezo huo yatakayofanyika kwenye fukwe za Lido Resort, Entebbe nchini Uganda kuanzia Novemba 25-26, mwaka huu.

Wachezaji hao waliochaguliwa ni Davis Neeke na Ford Edward kwa upande wa wanaume, wakati wanawake ni Evelyne Albert na Hellen Richard.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wavu Tanzania (Tava), Shukuru Chilonga, alisema timu ya Tanzania itaondoka nchini kati ya Novemba 20 hadi 22 ili waweze kuwahi na kuzoea mazingira.

“Kwa sasa wachezaji waliochaguliwa wanafanya maandalizi kwenye sehemu tofauti na walimu wao, huku Tava tukiwa karibu nao ili kuona jinsi wanavyojiandaa na jinsi gani tunatakiwa kuwasaidia kwa lengo la kufikia malengo.

“Tunakwenda Uganda kuwakilisha nchi lakini kizuri zaidi wenyeji wetu ndio wenye jukumu la kutugharamia kuanzia suala la chakula, malazi na usafiri wa ndani kwa siku zote tutakazokuwa huko,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.