KOCHA MPYA SIMBA AJIFUNGIA KUPIKA DAWA YA YANGA SC

Dimba - - Front Page - NA MWANDISHI WETU

KOCHA mpya msaidizi wa Simba, Masudi Djuma, alijifungua kuiangalia Yanga iliposhuka dimbani Jumapili iliyopita wakati wa mechi yao dhidi ya Stand United, iliyomalizika kwa Wanajangwani hao kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Kocha huyo wa zamani wa Rayon Sport ya Rwanda, alitua nchini Alhamis iliyopita kwa ajili ya kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Mganda Jackson Mayanja, aliyeachana na timu hiyo kwa madai ya kuwa na matatizo ya kifamilia. Kiongozi mmoja wa Simba aliliambia DIMBA Jumatano kwamba, alikuwa na kocha huyo sehemu tulivu wakifuatilia mchezo huo wa Yanga na Stand United, na tayari ameshasoma mbinu zao zote.

“Kweli aliufuatilia sana mchezo huo Yanga walipocheza na Stand United, na kubwa ni kwamba kuna baadhi ya wachezaji, akiwamo Ajib, alisema ni wa kuchungwa sana.

“Hata hivyo, baada ya mchezo huo kumalizika alisema anakwenda kushauriana na Kocha Mkuu Joseph Omog, namna ya kupanga kikosi chao kuelekea mchezo huo ambao ni muhimu kwetu kushinda,” alisema kigogo huyo. Kwa sasa Simba wamejichimbia Zanzibar, kujiwinda na mchezo huo, ambapo tayari homa ya mpambano huo imeshapanda kwa pande zote mbili, kwani Yanga nao wameamua kujificha mkoani Morogoro.

Nahodha wa timu ya Msimamo FC, Rajabu Kagawa (kushoto), akimdhibiti mchezaji wa timu ya Zaragoza FC, Karim Shukuru, wakati wa mchezo wa ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, iliyofanyika Dar es Salaam juzi, katika Viwanja vya Jakaya Kikwete. PICHA: IMANI NATHANIEL

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.