‘RONALDO AGAIN’

Dimba - - Front Page - LONDON, ENGLAND Tatu bora ya Fifa ilivyokuwa Kocha bora wa kike Tatu bora ya makocha wa kike Sarina

Cristiano Ronaldo - 43.16 % Lionel Messi - 19.25 % Neymar - 6.97% Tatu bora ya wanawake Lieke Martens - 21.72 % Carli Lloyd - 16.28 % Deyna Castellanos - 11.69% Gianluigi Buffon Dani Alves Leonardo Bonucci Marcelo Sergio Ramos Andres Iniesta Toni Kroos Luka Modric Lionel Messi Neymar Cristiano Ronaldo Tatu bora ya makocha Zinedine Zidane - 46.22% Antonio Conte - 11.62% Massimiliano Allegri - 8.78%

CRISTIANO Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa Fifa kwa mwaka 2017.

Hii ni tuzo ya pili mfululizo kwa straika huyu wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, akiwagaraza wapinzani wake, Lionel Messi na staa wa PSG, Neymar.

Lieke Martens wa Barcelona na timu ya taifa ya wanawake ya Uholanzi, alibeba tuzo ya mwanasoka bora wa kike kwa mwaka 2017.

Zinedine Zidane alibeba tuzo ya kocha bora wa mwaka wa FIFA kwa upande wa wanaume na kocha wa timu ya wanawake ya Uholanzi, Sarina Wiegman, akitwaa tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa wanawake.

Straika wa Arsenal, Olivier Giroud, alibeba tuzo ya bao bora la mwaka 2017, kwa bao la mtindo wa 'scorpion kick' alilofunga dhidi ya Crystal Palace, Januari.

Celtic kwa upande wao wamebeba tuzo ya klabu yenye mashabiki bora kwa mwaka 2017. Hapa tumekuandalia mchanganuo wa tuzo hiyo ulivyokuwa.

Ipi tofauti ya tuzo ya Ballon d'Or na hii ya Fifa?

Huu ni mwaka wa pili tuzo ya Fifa inatolewa kwa miaka ya hivi karibuni, ikitofautiana na tuzo maarufu za Ballon d'Or.

Tuzo za Ballon d'Or zilianzishwa na jarida la michezo la Ufaransa, lakini mwaka jana Fifa waliamua kujitenga na kuendeleza tuzo zao binafsi.

Mshindi wa tuzo ya Fifa hupatikana kwa kura za manahodha wa timu za taifa, makocha, waandishi wachache wanaoteuliwa na kura za mashabiki, zinazotumika kwa asilimia 25 kwenye matokeo ya jumla.

MCHEZAJI BORA WA KIUME - CRISTIANO RONALDO

Umekuwa mwaka wa mafanikio sana kwa Ronaldo, akiwa na mafanikio ya kuliongoza taifa lake la Ureno kubeba kombe la Euro, mwaka 2016.

Mwaka huu CR7 alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-2, walioupata Real Madrid mbele ya Juventus kwenye fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

Kama haitoshi, Ronaldo alifunga mabao 25 kwenye michezo 29 ya ligi na kuisaidia Madrid kubeba taji la kwanza la La Liga, katika kipindi cha miaka mitano.

"Tumekuja England kwa mara ya kwanza na nimeshinda kwa mara ya pili mfululizo. Hii ni heshima kubwa sana kwangu," alisema Ronaldo baada ya kubeba tuzo hiyo.

Kama ilivyo kawaida, Messi alipata kura ya mchezaji mwenzake wa Barcelona, Luis Suarez, huku Ronaldo akipata kura ya Luka Modric aliyeiwakilisha Croatia.

Kilichovutia zaidi ni kuwa kura ya kocha wa England, Gareth Southgate, ilikwenda kwa Ronaldo. Mchezaji bora wa kike - Lieke Martens Martens, (24), alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Uholanzi kilichobeba taji la Euro, kwa upande wa wanawake akiibuka mchezaji bora wa michuano hiyo.

Nyota huyu alimgaragaza mpinzani wake Carli Lloyd wa Marekani, aliyebeba tuzo hiyo mwaka 2016.

KIKOSI BORA CHA FIFA

Kumekuwa na mabadiliko matatu kutoka katika kikosi cha mwaka 2016. Mkongwe Gianluigi Buffon alimpindua Manuel Neuer, huku nafasi ya Leonardo Bonucci ikichukuliwa na Gerard Pique na Neymar akaingia kikosini badala ya Luis Suarez.

Kikosi kimekusanya wachezaji watano kutoka Real Madrid, wawili wa Barcelona, wawili wa PSG, mmoja kutoka Juventus na AC Milan. Hakuna mchezaji wa Premier League aliyeingia kwenye orodha hii.

KIKOSI BORA CHA MWAKA KOCHA BORA WA KIUME

Real walimaliza msimu uliopita kwa kubeba taji la ligi na kufanikiwa kutetea Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe hilo.

Zidane alistahili kubeba tuzo hiyo akimgaragaza Antonio Conte aliyetwaa taji la Premier League akiwa na Chelsea.

Kocha wa Uholanzi, Wiegman, aliliongoza vyema taifa lake kubeba taji la Ulaya, mwaka 2017 kwenye ardhi ya nyumbani, wakisifika kwa soka la kushambulia kwa kasi.

Tuzo ya bao bora la mwaka 2017, ilikwenda kwa straika wa Arsenal, Olivier Giroud.

Giroud alifunga bao hilo dhidi ya Crystal Palace, kwa staili ya 'scorpion' kick, akiunganisha krosi iliyochongwa na Alexis Sanchez.

Olivier Giroud alipata asilimia 36.1% ya kura 792,062 KIPA BORA WA MWAKA

Ana medali ya Kombe la Dunia, mataji 10 ya Serie A na sasa Gianluigi Buffon, anakuwa kipa wa kwanza kubeba tuzo hii ya Fifa.

Mkongwe huyu anayekipiga katika klabu ya Juventus, aliwasaidia Juventus, kubeba taji la Seria A, mara sita mfululizo huku akicheza kwa dakika 600 katika ligi ya mabingwa bila kuruhusu bao.

Buffon, (39), alibeba tuzo hiyo akiwagaraza wapinzani wake akiwamo Keylor Navas wa Real Madrid na Manuel Neuer aliyeisaidia Bayern Munich, kubeba Bundesliga.

"Hii ni heshima kubwa kwangu, si jambo dogo kubeba tuzo hii katika umri wangu," alisema Buffon.

Wiegman - 36.24% Nils Nielsen 12.64% Gerard Precheur 9.37% Bao bora la mwaka

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.