Singida United wapewa elimu ya Ujasiriamali

Dimba - - News - NA SALMA MPELI

KIKOSI cha timu ya Singida United pamoja na benchi zima la ufundi, kilitembelea Kampuni ya YARA Tanzania ambao ni wadhamini wao wakuu na kupewa elimu ya ujasiriamali wa kilimo na matumizi ya mbolea bora inayozalishwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na wanahabari wakati wa ziara hiyo, Meneja Mkuu wa YARA Tanzania, Alexando Masido, alisema lengo la kuwaita Singida United kutembelea kampuni hiyo ni kusaidia katika maendeleo ya wachezaji ambao wanapatiwa elimu ya ujasiriamali.

"Tunaendelea na kampeni yetu ya ‘Kijana stuka mtonyo shambani’, hivyo kupitia jambo hilo, Singida United kama walivyo vijana wengine wanapaswa kujua umuhimu wa kilimo na matumizi ya mbolea bora," alisema Masido.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.