Stars kuifuata Benin Novemba 9

Dimba - - News - NA MWANDISHI WETU

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga, ametaja kikosi chake ambacho kitajiandaa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin, utakaofanyika mwezi ujao nchini humo.

Kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Manula (Simba SC), Manyika Peter (Singida United) na Ramadhani Kabwili (Yanga). Mabeki ni Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons), Erasto Nyoni (Simba) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Kwa upande wa viungo Mayanga amewaita Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamiru Yassin (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Difaa El-Jadid), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Ajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) pamoja na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.