MAKONDA AKABIDHI VIFAA KIKAPU

Dimba - - Maoni - NA SHARIFA MMASI

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewakabidhi viongozi wa Chama cha Mpira wa Kikapu cha mkoa huo (BD) mabati 150, jenereta lenye uwezo wa Kv 35 pamoja na mipira 110.

Zoezi hilo la makabidhiano lililohudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwamo wachezaji wa kikapu, lilifanyika jana majira ya saa sita mchana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa, Ilala, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea vifaa hivyo, Rais wa BD, Emesu Okare, alimshukuru mkuu wa mkoa kwa msaada wake na kumwahidi kufanya kazi kwa juhudi ili mpira wa kikapu ulete heshima kwa Taifa.

“Tunashukuru kupata vifaa ambavyo tulikuwa na uhitaji mkubwa kwa ajili ya kufanikisha michezo na ndoto za vijana wetu.

“Tunaahidi mbele yako kuzidisha juhudi katika kuhamasisha vijana kuupenda na kushiriki mchezo huu na pia kuiletea nchi mafanikio kupitia kikapu,” alisema.

Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania, Adrian Nyangamale (kulia), na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Data Vision, William Kihula, wakibadilishana mikataba ya mradi wa Sanaa za Ufundi Tanzania Dar es Salaam jana (katikati) anyeshudia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na michezo, Juliana Shonza. Picha na Jumanne Juma

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.