Umati wa maafande wamnyima ushindi Minziro

Dimba - - Maoni - NA MAREGES NYAMAKA

UMATI mkubwa wa maafande wa Jeshi la Polisi ulipelekea kikosi cha Manispaa ya Kinondoni (KMC) kinachonolewa na kocha, Felex Minziro, kushindwa kupata matokeo mazuri ugenini dhidi ya Polisi Tanzania.

KMC ilijikuta ikiambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, mchezo uliopigwa Uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Minziro aliliambia DIMBA Jumatano kuwa, umati wa askari kutanda pembezoni mwa uwanja wakiwa na magari ya kipolisi zaidi ya 10 iliwatisha wachezaji na kucheza kwa hofu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.