Snura kuachia kali ya mwaka

Dimba - - Maoni - NA MWANDISHI WETU

STAA wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi, amebainisha kuwa, anatarajia kutoa ngoma kali ya kufunga mwaka kati ya Novemba au Desemba, ili kuendelea kukata kiu ya mashabiki wake.

Mkali huyo wa ‘Zungusha’, aliyomshirikisha Christian Bella, aliliambia DIMBA Jumatano kuwa, licha ya wimbo wake huo kuendelea kutesa sokoni, lazima aje na nyingine kali ya funga mwaka.

“Nashukuru ‘Zungusha’ imepata mwitikio mkubwa tangu nilipoitambulisha mwanzoni mwa mwezi huu, ninachokifanya sasa hivi ni kushusha ngoma nyingine kali ya kuaga mwaka wa 2017,” alisema.

Mwanadada huyo mwenye manjonjo mengi awapo jukwaani, ambaye ni mnazi mkubwa wa timu ya Simba, aliongezea kuwa, kila kukicha inabidi usome soko la muziki linahitaji nini ili kwenda na wakati.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.