BIL NAS

amfikiria Ali Kiba collabo ijayo

Dimba - - Maoni -

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya ngoma yake mpya ya ‘Sina Jambo’ kufanya vizuri, msanii wa kizazi kipya, William Lyimo, maarufu kama Bilnas, amesema anafikiria kufanya kazi na Ali Kiba kwa sasa, kutokana na kuwa miongoni mwa wasanii wanaokubalika zaidi kupitia kazi zao. Bil Nas aliliambia DIMBA kuwa, uwezo wa Kiba kufanya vizuri kwenye kila wimbo anaoshirikishwa ama anaofanya mwenyewe umemshawishi kwa kiasi kikubwa kumfikiria kwenye kazi yake ijayo. “Ali Kiba ni mmoja wa wasanii ninaowakubali sana uwezo wao, anafanya vizuri sana, hasa akishirikishwa kwenye ngoma za wasanii mbalimbali, nimekuwa nikimsikia nikiwa hata sijaanza muziki na hadi sasa amekuwa akifanya vizuri,” alisema Bilnas. Aliongeza kwa sasa baada ya ngoma yake ya ‘Sina Jambo’ kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa mashabiki, anajipanga kuachia wimbo mwingine, huku akifikiria zaidi kumshirikisha msanii huyo mkubwa na anayefanya vizuri kwa sasa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.