Mastaa wamchana Weinstein

Dimba - - Jumapili -

MNAMO Oktoba 5, mwaka huu, gazeti la New York Times lilichapisha habari ya uchunguzi kuhusu wanawake waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji na mtayarishaji wa Àlamu, Harvey Weinstein. Baadhi ya nyota wamefunguka kuhusu tabia za mkali huyo.

Hadi sasa zaidi ya wanawake watano wamekiri kukumbana na kadhia ya mkali huyo ambaye anatamba na kazi zake zenye ubora wa hali ya juu.

Angelina Jolie, mwigizaji wa kike, alisema: "Nina uzoefu mbaya dhidi ya Harvey Weinstein tangu nilipokuwa mdogo, ndiyo maana nilichagua kutofanya naye kazi na nilikuwa nikiwaonya wale waliokuwa wakihitaji kufanya kazi naye."

Gwyneth Paltrow, ambaye pia ni mwigizaji, aliliambia New York Times kuwa, alipokuwa na miaka 22, Weinstein alimfukuza kabla ya kuanza kazi mara baada ya kukataa mwaliko wake wa kwenda katika chumba cha hoteli aliyoÀkia.

Cara Delevingne, ambaye ni mwanamitindo na mwigizaji, alisema aliitwa katika kikao na Weinstein, katika moja ya hoteli wakiwa na mwongozaji mwingine, lakini baadaye walibaki wao wawili, lakini ajabu mtayarishaji huyo alikuwa akimshawishi kuingia katika chumba chake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.