Real Madrid: Jikolililopika mastaa wakubwa duniani

Dimba - - Jumapili - MADRID, HISPANIA

INATAMBULIKA wazi kuwa, Real Madrid ni moja kati ya klabu maarufu zaidi duniani, lakini ni wachache waliofanikiwa kugundua kuwa Los Blancos ina akademi bora ya kuzalisha vijana na inayoendelea kufanya hivyo hadi sasa. Wao pia wanatumia wachezaji waliowazalisha wenyewe; Dani Carvajal, Nacho na Lucas Vazquez, lakini kuna mastaa wengine kibao wanaosakata soka Ulaya, wakiwamo Juan Mata, Alvaro Morata, Juanfran na Borja Valero, nao pia waliibuliwa kwenye ngazi za vijana Madrid. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na shirika la utafiti wa masuala ya soka, CIES Football Observatory, ulidhihirisha kuwa, Madrid imezalisha wachezaji wengi zaidi wanaoendelea kucheza soka kwenye Ligi Kuu tano kubwa za Ulaya; Premier League (England), La Liga (Hispania), Serie A (Italia), Bundesliga (Ujerumani) na Ligue 1 (Italia), kuliko klabu yoyote ile.

Kuna wachezaji 41 ambao msingi wa soka lao ni kutoka kwenye klabu hiyo, ambapo wachezaji nane kati yao bado wanacheza kwenye kikosi cha kwanza cha Los Blancos hao.

Kama umezitazama mechi za Madrid hivi karibuni, bila shaka jina la Achraf Hakimi, 18, si geni kwako, kwani kinda huyo mzaliwa wa Madrid mwenye asili ya Morocco, ni mchezaji wa mwisho mwisho kuibuka hivi karibuni.

Wapinzani wa Madrid, Barcelona, wao wamezalisha nyota 34, saba kati yao wakiendelea kusaka soka kwenye dimba la Camp Nou, huku klabu ya Lyon ikifuatia kwa kuzalisha nyota 31 wanaosakata soka barani Ulaya.

Ni wachezaji 11 ambao wametokea kwenye akademi ya miamba hao wa soka la

Ufaransa, akiwamo staa wao, Nabil Fekir.

Bilbao Katika nao hali wamzalisha wachezaji wengi ykushangaz pia, Athletic ambao bado waacheza kwenye ligi tano kuu za Ulaya, waitajwa kufikia 29.

20 kati yaobado wapo San Mames, ikiwa ni sera maalumu ya klabu hiyo kuaji watumia wachewaliozaliwa kwenye mji wa Basque, Hispania, ambapo Bilbao wanaweka makazi yao hapo.

Man United inakamilisha timu tano kwenye orodha hiyo, kwa kuzalisha nyota 28 wanaocheza kwenye ligi yao, Hispania, Italia, Ujerumani au Ufaransa.

Cha kusikiti ha kwa mashabiki wa United waliozoea kuona nyota wao waliowaibua wenyewe wakiitumikia klabu hiyo, ni wachezaji wat no tu ambao bado wapo hapo.

Rennes ni klbu nyingine inayojulikaake na kwa uwezo wake wa kuzalisha wachea zaji wenye vipajina akademi yao ina jumla

ya nyota 22 ambao bado wanacheza kwenye ligi kubwa tano za Ulaya, akiwamo Tiemoue Bakayoko, aliyesajiliwa na Chelsea sambamba na winga wa Barcelona, Ousmane Dembele.

Arsenal wametajwa kuzalisha nyota 21, ambao waliwahi kuichezea klabu hiyo, lakini kwa sasa wapo kwenye klabu nyingine, kama ilivyo Monaco.

Klabu pekee nje ya Ulaya ambayo imeingia kwenye orodha hiyo ya timu 25 ni River Plate, ambapo miamba hao wa Argentina wamezalisha wachezaji 17 wanaocheza kwenye timu za ligi tano kubwa za Ulaya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.