Nigeria, Serbia zajinoa kuelekea Kombe la Dunia

Dimba - - Jumapili - LAGOS, NIGERIA

TIMU za Nigeria na Serbia zipo kwenye matayarisho ya kucheza mechi ya kirafiki kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018. Timu zote mbili zimefanikiwa kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi, ambapo mataifa hayo mawili yameona ni vyema kujiandaa mapema ikiwa ni njia ya kujitengenezea matokeo bora wakati wa fainali hizo.

Temi Gold, Rais wa Chemba ya wafanyabiashara wa SerbiaNigeria, ni miongoni mwa watu wanaotajwa kuendesha mpango huo ambao utakuwa na manufaa kwa pande zote huku madawati ya ufundi ya timu zote yakiafiki mpango huo.

Nigeria imepata nafasi ya kwenda Urusi 2018 baada ya kushinda katika Kundi B kanda ya Afrika huku Serbia ikishinda katika kundi D, kanda ya Ulaya.

Kikosi cha Nigeria

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.