Usiiangamize afya yako kwa kutumia dawa holela

Dimba - - Jumapili -

TUKUBALI tusikubali, lakini ukweli upo kwamba, idadi kubwa ya wanaume hivi sasa wanahangaika kutokana na kukumbwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, na idadi kubwa kati ya hao wameshaamua kutumia dawa aina ya viagra bila kupata maelekezo ya kitabibu, hali hiyo inaweza kuzidisha tatizo katika siku chache zijazo.

Matumizi ya dawa hizo yanaweza kuleta faraja kwa siku za mwanzoni, lakini baadaye yakaleta maafa makubwa ya mtu kushindwa kushiriki kabisa katika tendo hilo, hii inatokana na uholela unaotumiwa bila kufuata masharti.

Mbaya zaidi, wengi wanaotumia dawa hizo hufanya siri baina yao na wapenzi wao, lakini hawatambui kwamba watakabiliwa na aibu itakayowabidi wote wawili wakumbwe na fadhaa ya mabadiliko ya maisha yao.

Kimsingi kila anayepata na tatizo hili anapaswa kujulikana sababu, uzito kiasi gani, chanzo kilikuwaje na hali yake imeathirika kiasi gani, je, zipo nje za kuweza kurudidha hali sawa bila kutumia tiba na ni tiba ya aina gani na kiasi gani inastahili kutumiwa, vilevile zipo njia sahihi za kulifikisha tatizo hili nyumbani.

USIRI NI ADUI

Kama mke na mume ni watu wanaotakiwa kujuana na kufahamiana mambo yanayowazunguka kwa asilimia 99, basi suala la usiri kwao halipendezi na lisifanyike kabisa.

Bali kila yanapotokea mabadiliko, yawe ya mwili au kimaisha, basi kila mmoja awe mshiriki anayelifahamu tatizo kwa kina.

Kwa maana nyingine, isiwe siri ya mke au mume, kwani kwa kushirikiana kwao wangeweza kupata suluhisho la pamoja. TABIA HATARISHI Utafiti umegundua kwamba, njia zinazochangia kuwapo ongezeko la wanaume wanaokosa nguvu za kiume, ni aina ya vyakula.

Vipo vyakula vingi hivi sasa vinavyoliwa na watu wengi ambavyo ndani yake vina kemikali zinazosababishwa na mafuta ambavyo mara nyingi huchangia kuvuruga mfumo wa damu na kufanya mtu kupungukiwa na mambo fulani mwilini.

Inaweza isiwe nguvu za kiume pekee, bali hata kupata maumivu ya viungo, au baadhi ya sehemu za mwili kupata ganzi, na hasa wengi huikuta wakipata vitambi visivyokuwa rasmi vinavyoleta miungurumo isiyokuwa ya kawaida tumboni.

Hivyo basi vyakula vya asili na hata dawa za asili zipewe nafasi kutumika mara kwa mara.

Pia ulevi kupindukia, na kutokuwa na muda mrefu wa kupata mapumziko na hasa wale wanaofanya kazi ngumu huwa na hatari zaidi ya kupata hali hii isiyofurahisha katika jamii.

KUEPUKA HALI HII

Tunasema tiba ni hatua ya mwisho, inapokuwa sasa imeshindikana, lakini pia zipo njia mbadala kama vile kufanya mazoezi na kurudisha ratiba zako za mlo.

Kupata usingizi kwa muda mrefu, pia kuepuka kunywa pombe nyingi na kwa muda mrefu, maana tabia hii huuchosha mwili na kutengeneza usugu wa maradhi yaliyomo mwilini.

Unaweza ukazidisha hali ya ulevi ukajikuta pia unapata shida ya upumuaji, hii inakuja muda mfupi baada ya kuona hali ya ushiriki wako wa tendo la ndoa umebadilika.

Mazoezi ni tiba, usingizi ni tiba na heshima ya mlo wa asili wenye mchanganyiko wa matunda nao pia ni tiba, lakini hali ikizidi unapaswa kupata tiba sahihi, kwa maana nyingine, hali hii nisifichwe na ielezwe wazi na hata ikibidi mpenzi wako afahamu. Maoni na ushauri simu namba 0712 328223.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.