Chenji ya Ajib na Okwi inarudi kwa kasi kubwa

Dimba - - Jumapili -

EMMANUEL Okwi anafunga, Ibrahim Ajib anatupia. Mastraika hawa wawili kwa sasa ndio mhimili wa safu ya ushambuliaji ya vikosi vya timu zao za Simba na Yanga katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Okwi na Ajib ndio wanaokimbizana katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kwa mfungaji bora wa Ligi Kuu mwishoni mwa msimu. Kabla ya mechi ya jana baina ya timu hizo iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Okwi alikuwa ameshatikisa nyavu mara nane, wakati Ajib ameshaweka kambani mabao matano.

Moto wao wa kucheka na nyavu umewaweka katika vita kali ya kuwania ufungaji bora wa ligi hiyo. Kila mmoja amekuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu za Ligi Kuu. Okwi akifunga Ajib naye anamjibu kwa vitendo.

Thamani ya usajili wa wachezaji hao imeanza kuendana na kile wanachokifanya ndani ya timu zao. Okwi ni mchezaji ghali namba mbili ndani ya kikosi cha Simba, akiwa nyuma ya Haruna Niyonzima, anayeshika nafasi ya kwanza katika orodha ya wachezaji waliosajiliwa na klabu hiyo msimu huu.

Mbali na dau nono la usajili alilopewa na Simba kukamilisha mipango ya kumtoa SC Club Villa ya Uganda msimu huu, pia Okwi ni mchezaji anayepokea mshahara mnono miongoni mwa nyota wa kikosi cha Simba.

Usajili wa Ajib kutoka Simba kwenda Yanga umeigharimu klabu hiyo kiasi cha Sh mil 60, huku pia akitengewa mshahara mnono unaomuweka katika tatu bora ya wachezaji wanaovuta mkwanja wa kutosha kila mwisho wa mwezi. Miguu na vichwa vya wawili hawa vinatenda haki. Viungo hivyo viwili vya mastraika hao ni tishio kwa mabeki na makipa wa timu pinzani. Okwi na Ajib wamejitofautisha katika mambo mawili mpaka sasa.

Ajib amekuwa mtamu ndani ya kikosi cha Yanga, akionyesha umahiri wa kufunga mabao kwa kutumia miguu yake, wakati Okwi anatupia kwa vichwa zaidi. Mipira ya faulo za Yanga inayopigwa na Ajib imewaaminisha mashabiki wa timu hiyo kuwa asilimia kubwa lazima itatinga nyavuni. Hili limemfanya Ajib kuaminiwa naye kuwaaminisha kwa kupiga mipira mingi ya faulo ambayo timu yake imekuwa ikipata kwenye mechi za Ligi Kuu. Kwa bahati nzuri, nafasi nyingi alizopata za kupiga faulo zimekuwa zikiamsha shangwe za kushangilia bao kwa Yanga. Hili limemjengea heshima na mapenzi kwa mashabiki wa timu hiyo.

Mtazame Okwi namna anavyoitendea haki mipira ya krosi anayochongewa

Ajib amekuwa mtamu ndani ya kikosi cha Yanga, akionyesha umahiri wa kufunga mabao kwa kutumia miguu yake, wakati Okwi anatupia kwa vichwa zaidi. Mipira ya faulo za Yanga inayopigwa na Ajib

na wenzake.

Amekuwa mjuzi wa kujua namna ya kujipanga na kufunga kwa kutumia kichwa chake.

Kila krosi inayopigwa yupo na kuhakikisha anafunga au kuwapa hofu mabeki wa timu pinzani kulazimika kumchunga wawili wawili. Hili limewapa furaha mashabiki wa Simba, wakiamini hakuna kama Mganda huyo kwenye safu yao ya ushambuliaji.

Wawili hawa, mbali na kufunga, pia wamekuwa wazuri kwenye kupiga chenga na kupiga mabao ya timu zao yanayofungwa na nyota wengine. Nani anayeweza kubisha umahiri alionao Ajib ndani ya kikosi cha Yanga, lakini pia Okwi kwa Simba. Ajib na Okwi wamekuwa wakizipa matokeo bora Simba na Yanga katika hali yoyote. Nyota hawa wawili wamejipambanua uwezo wao wa kufunga hata kwa juhudi zao binafsi pale inapotokea timu yao imekamatwa na wapinzani. Kuna nyakati wamekuwa wakifunga mabao katika mazingira magumu.

Uwezo binafsi wa mchezaji umekuwa na nafasi yake kwenye kusaka matokeo. Simba na Yanga zinachekelea usajili wa nyota hawa. Hawana walichopoteza kwenye pesa waliyotoa kukamilisha usajili wao. Ni mwendawazimu pekee anayeweza kujipa ujasiri wa kuwatazama nyota hawa, si msaada mkubwa kwa timu zao. Kazi kubwa ya miguu na vichwa vyao imeongeza thamani yao.

Ni dhahiri wameanza kurudisha chenji ya gharama za usajili zilizotumika kuwasajili. Tusubiri kuona mengi kupitia miguu na vichwa vyao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.