Jurgen Klopp: Man City ‘mabingwa’ ikifika Januari

Dimba - - Jumapili - MERSEYSIDE, England

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, ameukubali mziki wa Manchester City na amekiri kuwa huenda timu hiyo ikatangazwa mabingwa wa Premier League mapema mwakani.

City imekuwa na kiwango kilali msimu huu na jana iliendeleza ubabe kileleni kwa kuinyuka West Brom mabao 3-1 ugenini na kufikisha pointi 28 baada ya kushinda mechi tisa kati ya 10 walizocheza hadi sasa na hawajafungwa mchezo wowote.

Liverpool, inakamata nafasi ya sita kwenye msimamo, pointi 12 nyuma ya City.

“Ukiwaangalia City kwa sasa ni kama watachukua ubingwa Januari au mwezi mwingine. Wanaonekana kuifanya kazi yao kwa ufasaha na haina budi kumheshimu wapinzani wako kwa kazi nzuri wanayoifanya,” alisema.

Liverpool nao waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Huddersfield jana, na kufikisha pointi 16, mabao yakifungwa na Daniel Sturridge, Roberto Firmino na Giorginio Wijnaldum.

Matokeo mengine jana ni kama ifuatavyo; Crystal Palace ilitoshana nguvu 2-2 na West Ham, Watford ikachapwa 1-0 na Stoke huku Arsenal wao waliiadabisha Swansea 2-1.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.