‘Maisha bila Kante mbona fresh tu’

Dimba - - Jumapili -

KAMA ulidhani Chelsea itahangaika kisa N’Golo Kante hayupo, basi utakuwa unakosea, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo, Antonio Conte, maisha yatazidi kusonga mbele darajani licha ya kwamba kiungo huyo hayupo dimbani.

Conte alisisitiza kuwa Chelsea ina uwezo wa kuendelea na safari bila kumtegemea Kante ambaye amezikosa mechi nne tayari kutokana na maumivu ya paja yanayomsumbua na anatarajiwa kurudi hivi karibuni.

Katika muda wote huu, The Blues wameruhusu mabao nane na wakati Conte akitambua wazi umuhimu wa kiungo huyo, bado anaamini kuwa Chelsea ni zaidi ya Kante.

“Niwe mkweli, bila Kante mambo huwa ni magumu. Ni mchezaji muhimu kwetu lakini nadhani timu kwa sasa inaendelea kucheza vizuri bila yeye,” alisema Conte.

Aliongeza: “Natumai kumwona uwanjani hivi karibuni ila kuna wachezaji wengine nimewaona wapo kama Kante. Wanatusaidia. Lakini sote tunajua kuwa N’Golo ni mchezaji mzuri sana, kwa kujituma kwake anazidi kuwa mchezaji bora lakini wapo wengine bora kama yeye.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.