AISHI MANULA NI HABARI NYINGINE

Dimba - - Mbele - NA MWANDISHI WETU

AMA kweli Aishi Manula akiitwa ‘Tanzania One’ anastahili, kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha, ambapo kama isingekuwa yeye, huenda Simba wangepata matokeo mabaya dhidi ya Yanga.

Manula alichomoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Yanga, na kama angekuwa kipa legelege, ni wazi mashabiki wa Simba wangeondoka uwanjani vichwa chini.

Manula alionyesha uwezo wake katika dakika ya 23 ya mchezo huo, baada ya Geofrey Mwashiuya wa Yanga kuachia shuti kali na kipa huyo akaupangua mpira ukamkuta Papy Tshishimbi, ambaye naye aliachia shuti kali likapaa juu.

Katika dakika ya 30, Manula alifanya tena kazi ya ziada kuokoa mchomo wa Tshishimbi, baada ya kuachia shuti kali na kipa huyo alikaa vizuri na kuutoa mpira ukawa kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda.

Kama hiyo haitoshi, Manula alifanya tena kazi ya ziada kukabiliana na Mwashiuya, ambaye alikuwa amewazidi ujanja mabeki wa timu pinzani na kuutoa mpira ukawa kona ambayo haikuzaa matunda, huku pia akizuia mchomo wa Emmanuel Martin dakika za lala salama.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.