Jezi za Okwi, Ajib zauzwa kama njugu

Dimba - - Jumapili - NA SAADA SALIM

JEZI za straika wa Simba, Emmanuel Okwi na mwenzake wa Yanga, Ibrahim Ajib, jana ziligeuka lulu uwanjani kutokana na mauzo yake kuwa makubwa tofauti na za wachezaji wengine.

Utafiti uliofanywa na DIMBA, ulionyesha kwamba, jezi hizo ndizo zilizokuwa zimevaliwa na idadi kubwa ya mashabiki.

Okwi na Ajib ndio wachezaji ambao kwa sasa wamegeuka lulu kwa timu zao kutokana na aina ya uchezaji wao, wakifunga mabao na kuzifanya timu hizo kuondoka na pointi tatu muhimu.

Katika hatua nyingine jana wakati timu zinaingia uwanjani, Yanga ndio waliokuwa wa kwanza wakishuka kwenye gari lao saa 8:30 mchana na baada ya dakika tatu gari la Simba nalo liliingia.

Mchezaji wa kwanza kushuka kwenye gari kwa upande wa Yanga, alikuwa Ibrahim Ajib na kwa upande wa Simba alikuwa kiungo Mghana, James Kotei.

"Pointi moja tuliyoipata katika mchezo huu si ya kudharau imetusogeza mbele na tunaangalia sasa mehi yetu ijayo dhidi ya Mbeya City ili tuweze kujiweka vizuri katika mikakati yetu ya kuwania ubingwa msimu huu" alisema Omog.

Simba watasafiri kwenda jijini Mbeya ambako watakipiga na Mbeya City, katika mchezo utakaopigwa Novemba 5, Uwanja wa Sokoine.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.