Shabiki wa Yanga akiona cha moto Uhuru

Dimba - - Jumapili - NA SALMA MPELI

SHABIKI aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Ngwesa, anaweza asithubutu kurudi tena uwanjani, baada ya kupokea kipigo kikali kutoka kwa mashabiki wa Simba baada ya kujichanganya kwao akiwa amevaa tisheti ya rangi ya njano.

Shabiki huyo alipokea mkong'oto wa maana mpaka pale askari walipokwenda kuamulia huku wenzake wa Yanga nao wakifuata kutaka kuzipiga kavukavu na wenzao hao wa Simba.

Shabiki mwingine wa Simba naye nusura akipokee kichapo kutoka kwa mashabiki wa Yanga, baada ya kukatiza mitaa ya Wanajangwani hao wanapokaa akiwa amevaa jezi nyekundu na kilichomnusuru ni kutokana na kuwa karibu na askari.

Katika hatua nyingine uwanja huo wa Uhuru, haukuwa umejaa sana kama ilivyokuwa imetarajiwa ambapo inadaiwa wengi wameacha kwenda wakihisi wanaweza kukosa nafasi ya kukaa wakaamua waangalie kwenye televisheni tu.

Mchezo huo ulilazimika kuchezwa Uwanja wa Uhuru, kutokana na Uwanja wa Taifa, kuwa kwenye matengenezo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.