Joseph Omog: Ilikuwa mechi ya presha

Dimba - - Jumapili - NA SAADA SALIM

LICHA ya Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog kukiri kwamba mastraika wake walipata nafasi nyingi za kufunga dhidi ya Yanga lakini wakakosa umakini, kamwe hakukidharau kikosi cha Yanga na kudai kwamba kilicheza kwa ushindani na kuufanya mchezo uwe wa presha kwa dakika zote 90.

Timu hizo ziliumana jana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzungumko wa nane uliopigwa Uwanja wa Uhuru na kupatikana matokeo ya sare ya bao 1-1 na hivyo kuirejesha Simba kileleni katika msimamo wa ligi hiyo kwa kutimiza pointi 16 sawa na Yanga na Azam FC, lakini ikiongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Omog aliliambia DIMBA muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo kwamba, timu yake iliingia kwa tahadhali kubwa kutokana na historia ya mechi za timu hizi na kwamba sare hiyo ya kufungana bao 1-1, iliyowapa pointi moja ameipokea vizuri kwani imewasogeza mbele .

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.