Nne za Zone 5 kushiriki ‘Fiba Afrika’

Dimba - - Jumapili - NA SHARIFA MMASI

JUMLA ya timu nne zilizoshika nafasi ya juu kwenye michuano ya kikapu ya Kanda ya Tano (Zone 5) iliyomalizika hivi karibuni jijini Kampala, Uganda, zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Afrika maarufu kama Fiba Afrika, Novemba 10 mwaka huu nchini Angola.

Timu hizo ni mabingwa wanaume City Oilers ya Uganda, Patriots ya Rwanda, KPA pamoja na Equity zote kutoka Kenya.

Ikumbukwe kuwa michuano hiyo itakayoshirikisha jumla ya kanda sita, ina lengo la kusaka timu bingwa upande wa wanaume na wanawake, kuwakilisha Bara la Afrika kwenye mashindano ya dunia hapo baadaye.

Kwa mara nyingine tena, Tanzania tunaikosa nafasi ya kushiriki Fiba Afrika, baada ya timu tatu ambazo ni JKT, Savio pamoja na DB Lioness kushindwa kufanya vema Zone 5, kule nchini Uganda.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.