Nyota gofu apania makubwa ‘Kili Gofu’

Dimba - - Jumapili - NA SHARIFA MMASI

MCHEZAJI wa kulipwa (professional) wa klabu ya gofu Arusha, Nuru Molel, ameapa kuibuka kidedea dhidi ya mpinzani wake, katika mashindano makubwa ya Kili Gofu yanayotarajiwa kutimua vumbi Novemba 10 mwaka huu, mkoani Arusha.

Akizungumza na DIMBA jana, Nuru alisema kwa sasa anaendelea na mazoezi makali ya asubuhi na jioni, kujihakikishia ushindi huo.

“Arusha kuna hali nzuri sana ya ubaridi inayoweza kumsaidia mchezaji kufanya mazoezi kwa muda mrefu bila kuchoka.

“Binafsi naendelea na maandalizi kuelekea Kili Gofu, nimejipanga kuibuka kidedea dhidi ya wachezaji wote wa timu pinzani watakaoshiriki,” alisema Nuru.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.