RUBBY

aingia anga za Yemi Alade

Dimba - - Jumapili - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa muziki Bongo, Hellen George maarufu kama Rubby, amesema ni mapema kuzungumzia colabo yake na msanii mkubwa wa Nigeria, Yemi Alade, ingawa kwa sasa wapo kwenye mazungumzo mazuri. Mwimbaji huyo ameeleza kuwa hawezi kuweka hilo wazi kwani mipango yake sasa ni kuvunja ukimya wake kwa upande wa nyumbani baada ya wengi kudai amekua kimya kwa muda mrefu. “Siwezi nikasema tayari kila kitu kimemalizika, lakini vitu vipo na vinaendelea vizuri, sitaki kusema kabisa kwenye kolabo za kimataifa natamani iwe surprise kwa sababu nimekaa muda mrefu kimya na sasa nataka nirudi kivingine na kuwashangaza wengi ambao wanaamini nimepotea kimuziki,” alisema Rubby. Rubby ameongeza kuwa amekuwa akitumia muda mwingi kuhakikisha jina lake kwenye muziki halipotei na sasa anataka kuja na kazi mpya ambayo itamtambulisha kivingine kwenye soko la burudani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.