Darassa kuja na funga mwaka

Dimba - - Jumapili - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Shariff Thabeet maarufu kama Darassa, amezungumzia ujio wake mpya na kuahidi utakuwa mkali zaidi ya ngoma yake ya ‘Muziki’ aliyofungia mwaka jana.

Rapa huyo ambaye mara mwisho alisikika na ngoma ‘Hasara Roho’, amesema yupo katika maandalizi ya kufanya hivyo ila kwa sasa asingependa kulizungumzia sana kwani yeye siku zote si mwongeaji zaidi ya kufanya kazi.

“Kwenye single mpya watu wananijua mimi si mtu wa kuongea ongea kama sina kitu cha kuongea mara nyingi huwa nakuja kuongea nikiwa na kitu, kwa sasa naandaa project ambazo naamini nitakuja kufunga nazo mwaka, watu wakae tayari tunakuja tuko poa kabisa,” alisema Darassa.

Mwishoni mwa mwaka jana, Darassa alifunga mwaka na ngoma ya ‘Muziki’ ambayo alimshirikisha Ben Pol na inatajwa kuwa ndiyo ngoma pekee kufanya vizuri kutoka kipindi hicho hadi mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.