KVC waja na ‘Ongeza Mapenzi Zaidi’

Dimba - - Jumapili - NA GLOY MLAY

KUNDI la KVC Mauzo Stars, limeachia ngoma mpya iliyofanywa kwenye studio ya Burne Record inayoitwa ‘Ongeza Mpenzi Zaidi’, wakimshirikisha Beka Fleva.

Akizungumza na DIMBA jana, kiongozi wa kundi hilo, Ezra Mkuluku maarufu kama Eze B, pamoja na wasanii wanaounda kundi hilo, Richard Mlemwa (G.Mob) na Deus Mkuluku (Mr. Deo), alisema ngoma hiyo itaendelea kuwatambulisha vyema katika tasnia hiyo baada ya kimya cha muda mrefu.

“Tumekuja na ngoma hiyo ambayo tunaamini itafanya vizuri kutokana na tumemshirikisha mkali wa Bongo Fleva, Beka, tunawaomba mashabiki waendelee kutusapoti kwa sababu tumerudi upya kwenye game,” alisema.

Alisema wapo mbioni kufungua studio kwa ajili ya wasanii chipukizi ambao wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya kurekodi katika studio

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.