Hamilton apania kufuata nyayo za Senna

Dimba - - Jumapili -

MKALI anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora katika mchezo wa mbio za magari yaendayo kasi, Langalanga, kwa upande wa wanaume, Lewis Hamilton, amesema anaamini atafuata nyayo za mtu aliyemvutia katika mchezo huo, Ayrton Senna. Bingwa huyo mwenye umri wa miaka 32, aliingia katika mbio za magari mara baada ya kuvutiwa na uwezo uliokuwa ukionyeshwa na Senna, aliyefariki mwaka 1994, ambaye alishinda mataji matatu ya San Marino Grand Prix.

Hamilton amekuwa akimfuatilia Senna tangu alipokuwa mtoto kutokana na uwezo wa hali ya juu aliokuwa akiuonyesha bingwa huyo wa muda wote wa Formula One.

Mwingereza huyo atakuwa na kibarua kizito leo katika jiji la Mexico City, ambapo anatarajia kudhihirisha ubora wake mbele ya hasimu wake wa muda mrefu, Sebastian Vettel .

Iwapo nyota huyo atatwaa taji hilo, ataongeza idadi ya mataji katika kabati lake, kwani hadi sasa amebeba mataji ya Canadian GP pamoja na United States Grand Prix.--

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.