MTAKE MSITAKE

Hili Kombe la Carabao lishabebwa na Manchester

Dimba - - Jumapili - MANCHESTER, ENGLAND

SHUKRANI kwa michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Urusi mwakani, Carabao Cup ya mwaka huu tayari imeshaandaliwa kabati mjini Manchester, kazi ni kwa Man Utd au Man City kuliwania. Timu hizo mbili zilitinga robo fainali wiki iliyopita, ambapo United imepangiwa kuchuana na Bristol City, huku Man City wao wakitajwa kucheza na Leicester lakini timu hizo hazina haja ya kuumiza sana kichwa kwani mmojawapo atalinyakua taji hilo msimu huu. Unajua kwanini, tulia uelezewe… Man United ina rekodi ya kushangaza ambapo imeweza kunyakua taji hilo katika misimu miwili ya Kombe la Dunia, huku Man City ikifanya hivyo kwenye msimu mmoja.

Chini ya utawala wa Kocha Sir

Alex Ferguson, umahiriwa Cristiano Ronaldo na makali yakufumania nyavu kutoka kwa Ruuvan Nistelkamatiki. van Nistelkamatiki. rooy, United ilikuwa hai kumatiki.

Msimu wa 2005-06, ndio ambao United ililinyakua kombe hilo la ligi.

Vijana wa Fergie walitembeza vichapo kwa timu za larnet, West Brom, Birmingham na Blackburn na kufanikiwa kutinga fainali waliyochandika uana na Wigan na kuiandika ma bao 4-0 katika dimba laMillennium Cardiff, Wales.

Miezi minne baaday nyota kad-

haa wa Man United walikwea pipa kuelekea nchini Ujerumani kwa ajili ya kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2006.

Miaka minne iliyofuatia, Man United ililitwaa tena taji hilo kabla Kombe la Dunia 2010 halijaanza kutimua vumbi nchini Afrika Kusini.

Msimu huo, Wayne Rooney ndiye alikuwa staa mkubwa kwa kuifungia Man United mabao 34 katika michuano yote.

Bado wakiwa chini ya utawala wa Ferguson, Man United waliitafuta njia ya kutinga fainali kwa kuzitandika Wolverhampton, Barnsley, Tottenham na Man City, ambapo walipambana dhidi ya Aston Villa na kushinda kwenye Uwanja wa Wembley.

Rooney ndiye alikuwa shujaa wa Man United katika fainali hiyo kabla ya kukwea pipa kuelekea Afrika Kusini.

Kabla watu hawajapumzika vizuri, Kombe la Dunia tena hili hapa! 2014, Man City wakalibeba.

Vijana hao waliokuwa chini ya Manuel Pellegrini, walitinga fainali ya Kombe la Ligi baada ya kuzinyuka Wigan, Newcastle, Leicester na West Ham kwa jumla ya mabao 9-0.

Katika fainali City iliisasambua Sunderland mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Wembley, shukrani kwa mabao ya Yaya Toure, Samir Nasri na Jesus Navas, ikitoka nyuma bao moja lililofungwa na Fabio Borini.

Baada ya kubeba taji hilo, mastaa kibao waliiacha anga ya Ulaya na kutua Brazil kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka huo.

Tukirudi sasa kwenye mwaka huu, klabu hizo za Manchester, mmojawapo ana nafasi kubwa ya kwenda Urusi akiwa na furaha ya kushinda Kombe la Ligi.

Zaidi ya yote, timu hizo zinaonekana kupangiwa timu nyepesi ambazo watazitumia kama ngazi ya wao kusonga mbele.

Kama wakishinda wote, huenda wakakutana kwenye nusu fainali ambayo ina mechi ya nyumbani na ugenini au, kama wasipokutana mapema, basi fainali ya Februari 25 itawahusu.

Na kwa klabu moja ya Manchester kushinda taji hilo, itafanya rekodi iendelee kudumu zaidi na zaidi...

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.