Eto’o ahimiza amani Kenya

Dimba - - Jumapili - PARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Samwel Eto’o, amesisitiza kupatikana kwa hali ya amani barani Afrika hasa kwenye nyakati ambapo uchaguzi unafanyika huku akiitaja Kenya kuwa ni taifa linalotakiwa kudumisha amaniili mchezo wa soka uendelee mbele.

Nyota huyo ambaye alishazitumikia Barcelona, Real Madrid na Inter Milan kwa nyakati tofauti, amesema kwamba siasa haitakiwi kuingilia michezo lakini kama hakuna amani na usalama wa kutosha ni ngumu michezo kuendelea. "Siuala la amani ni muhimu sana, naamini katika kutafuta suluhu lazima nchi husika ziangalie jambo hilo kwa umakini kwa sababu ndicho kiini cha maendeleo ya michezo.

"Tumeona jinsi ambavyo michuano ya Chan kwa mwakani ilivyohamishwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) baada ya kuona hali ya kisiasa nchini Kenya ni yakutia mashaka.

"Naomba viongozi wa Afrika waelewe umuhimu wa amani na maendeleo ya Afrika katika soka, kwa hiyo nichukue nafasi hii kusisitiza amani barani Afrika, lakini niwatakie kila la kheri wenzetu wa taifa la Kenya wanaoendelea na uchaguzi wa marudio," amesisitiza nyota huyo.

Kenya ilikuwa mwenyeji wa michuano ya Chan mwaka 2018, lakini ilinyang’anywa kutokana na kuyumba kwa hali ya kisiasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.