Gervihno awashangaa wabaguzi

Dimba - - Jumapili -

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast anayekipiga katika kikosi cha Hebei China Fortune ya China, Gervais Lombe Yao Kouass 'Gervinho' (pichani), amewashangaa watu ambao wanaendekeza ubaguzi wa rangi katika zama hizi.

Gervinho ameviambia vyombo vya habari nchini China kwamba suala la ubaguzi wa rangi katika zama hizi ni ujinga uliopitiliza na unastahili kulaaniwa na watu wote.

"Nashangaa hadi leo hii kwa watu ambao wanasema wamestaarabika bado wapo baadhi yao wanaamini katika ubaguzi wa rangi, ni mambo ya ovyo, hayapendezi na yanastahili kulaaniwa kwa sababu hatutaki kuona yakiendelea kutokea katika dunia ya sasa," amesisitiza Gervinho nyota wa zamani wa klabu za Arsenal ya England, Roma ya Italia na Lile ya Ufaransa.

Licha ya vitendo vya kibaguzi kupungua kwenye michezo, lakini bado mchezo wa soka unatajwa kuwa ni sehemu za michezo yenye kiwango kikubwa cha watu wenye itikadi za kibaguzi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.