Zanaco FC yatamba kileleni

Dimba - - Jumapili -

TIMU ya Zanaco FC ya Zambia (pichani), imeendelea kutamba kileleni mwa Ligi Kuu ya Zambia baada ya kuongoza kwa kufikisha pointi 60 katika msimamo baada ya kucheza mechi 32.

Timu hiyo ambayo ni moja ya timu kubwa na yenye wachezaji bora, inaongoza ligi huku mpinzani wake, Green Buffaloes akiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 32.

Pamoja na kufanya vizuri lakini bado Zanaco haiwezi kujitangazia ubingwa kwani bado zimesalia mechi tatu hadi nne hivyo timu yoyote inaweza kutwaa ubingwa ikiwamo Zesco United yenye pointi 56 baada ya kucheza mechi 30.

Timu inayoburuza mkia ni City of Lusaka FC, baada ya kucheza mechi 31 na kufanikiwa kupata pointi 15 katika ligi hiyo yenye timu 20.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.