Majukumu matatu ya mwamuzi wa kati

Dimba - - Jumapili - Kwa maswali, maoni na ushauri katika sheria hizi 17 za mpira wa miguu, tuwasiliane kupitia barua pepe " kokudavid83@yahoo.com

KATIKA mchezo wa mpira wa miguu, mwamuzi wa kati ana majukumu mengi, lakini haya ni yale makuu matatu ya msingi, ambayo kwa mujibu wa sheria, ni lazima ayatekeleze wakati wa mechi.

Soka ina sheria zake ambazo zipo 17, ambapo sheria namba tano ndiyo inayomzungumzia mwamuzi wa kati pamoja na majukumu yake katika mchezo husika.

Majukumu hayo ya mwamuzi wa kati ni kabla ya mchezo, wakati wa mchezo pamoja na baada ya mchezo.

Jukumu la mwamuzi kabla ya mchezo anatakiwa kukagua vifaa vya wachezaji wa timu zitakazokuwa zinacheza katika mchezo husika atakaousimamia kwa wakati huo kuhakikisha hazifanani, kukagua mipira itakayotumika wakati wa mechi husika.

Pia ana jukumu la kukagua uwanja kama nyavu hazijalegea wala kutoboka, milingoti ya magoli na ile ya vibendera kama ipo imara, ikiwa ni pamoja na alama zote za uwanja zinaonekana vizuri. Aidha, majukumu yake mengine ni kuanzisha mchezo, kutunza muda, kutunza kumbukumbu pamoja na kutoruhusu watu wasiohusika kuingia uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo, ikiwa ni pamoja na pindi mchezo unapoendelea.

Wakati wa mchezo, mwamuzi ana jukumu la kusimamia sheria kwa kushirikiana na waamuzi wasaidizi wake, pia anaweza kuahirisha mchezo iwapo atabaini kuna uvunjifu wa amani uwanjani au uvunjifu mkubwa wa sheria kwa upande wa wachezaji pindi mchezo unapoendelea. Kama kutakuwa na mchezaji aliyeumia wakati wa mchezo na anahitaji kutibiwa nje ya uwanja, anaweza kuusimamisha mchezo huo kwa muda ili akapatiwe matibabu na atauanzisha tena mchezo kwa kuudundisha (dropping the ball) katika eneo lilelile alilousimamishia.

Jukumu lingine wakati wa mchezo ni kuhakikisha mchezaji aliyeumia hadi kutoka damu haendelei na mchezo hadi atakapopatiwa matibabu na iwapo sare yake itakuwa imechafuka kwa damu hatamruhusu kuendelea kucheza nayo na badala yake atamtaka akabadilishe.

Katika jukumu lingine wakati wa mchezo, mwamuzi anaweza kujizuia kutoa adhabu kwa mchezaji aliye katika nafasi ambayo itamfaidisha kwa maana ya kuweza kufunga goli, anakaribia kufunga goli au hata kama kafunga goli, lakini awali alikuwa kacheza faulo, ambayo haikusababisha madhara kwa mchezaji mwenzake.

Pia wakati wa mchezo mwamuzi huyo ana jukumu la kuwaadhibu wachezaji ambao ni watovu wa nidhamu kwa kadi za njano au nyekundu, kulingana na kosa, ikiwa ni pamoja na kutoa maamuzi kutokana na ushauri wa mwamuzi msaidizi kwa makosa ambayo atakuwa hajayaona. Jukumu lingine wakati wa mchezo anaweza kumbadilisha mwamuzi wake msaidizi iwapo ataona anamwingilia majukumu yake ya kazi kwa mujibu wa sheria. Kwa upande wa majukumu, baada ya mchezo, mwamuzi huyo wa kati anatakiwa kuandika ripoti ya mchezo na kuiwasilisha kwenye kamati na ataiwasilisha kwa mujibu wa kanuni zinavyosema.

Kanuni za ligi kuu zinamtaka mwamuzi huyo kuwasilisha ripoti ya mchezo ndani ya masa 48.

Uchambuzi huu umeandaliwa na mwandishi wa gazeti hili ambaye pia ni mwamuzi wa mpira wa miguu daraja la pili taifa.

Katika jukumu lingine wakati wa mchezo, mwamuzi anaweza kujizuia kutoa adhabu kwa mchezaji aliye katika nafasi ambayo itamfaidisha kwa maana ya kuweza kufunga goli, anakaribia kufunga goli au hata kama kafunga goli, lakini awali alikuwa kacheza faulo, ambayo haikusababisha madhara kwa mchezaji mwenzake. Pia wakati wa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.