Ukijua lugha ya mahaba utafurahia uhusiano

Dimba - - Jumapili - kiu yako. Sasa tazama lugha hizo.

WAKATI fulani unaweza kuwa na hamu ya kuwa karibu na mwenzi wako, lakini ukashangaa anajiweka mbali nawe. Hii inaweza kuwa kwa wote, wanawake na wanaume, lakini ukweli ni kwamba wanawake ndio wanakutana zaidi na tatizo hili. Utakuta mwanamke anataka kuwa karibu na mwenzi wake faragha lakini kutokana na sababu ambazo hazifahamu, anashangaa mwenzake anakaa mbali naye. Je, umewahi kujiuliza hilo? Hapa katika mada hii nitaeleza mambo ya msingi kwa mwanamke kuzingatia ili mwenzi wake aweze kuonyesha ushirikiano wawapo faragha na kufurahia kwa pamoja. LUGHA YA MAHABA Mnapokuwa chumbani lazima lugha ya mapenzi itumike, chumbani ni kama mpo katika nchi nyingine yenye lugha nyingine na sheria nyingine, ila wapo wanaokuwa hawajapitisha sheria hizo katika uhusiano wao. Wapo wanandoa wanaoishi na wenzi wao kwa muda mrefu lakini akihitaji penzi huogopa kumwambia mzee. Huu ni ulimbukeni ingawa inawezekana kulingana na mazingira ukashindwa kumwambia mzee unamhitaji. Zipo lugha za mapenzi ambazo ukizitumia bila kumwambia mzee moja kwa moja atakuelewa na kukata

LUGHA YA MAVAZI

Mavazi maalumu ya faragha ni moja ya lugha ya mapenzi inayotakiwa kuzungumzwa chumbani. Wengi wamekuwa na mazoea ya kuvaa suruali, sketi fupi au khanga wakati wa kulala. Hii ni sawa, lakini siku ambayo unahitaji kukumbatiwa na mwenzi wako lazima uonyeshe kuwa unahitaji.

Ukweli upo wazi kwamba, mwanaume akimhitaji mwanamke ni rahisi tu, kwa sababu ataonyesha dalili bila kusita au wakati mwingine atakuambia moja kwa moja. Kwa upande wa wanawake ni vigumu, lakini kwa kutumia mavazi ni rahisi sana.

Mavazi yakitumika kwa ubunifu chumbani husaidia kuamsha hisia! Kwa mfano kutumia khanga nyepesi, night dress nk. Sasa basi ni jinsi gani utapangilia mavazi hayo ili yalete hamasa?

Wanawake wengi hasa walioolewa wakishakaa ndani ya ndoa na kumzoea mwanaume huamua kujivalia mavazi yoyote ili mradi akiamini kuwa mume ameridhika naye, kumbe si kweli.

Mwanamke unahitaji ubunifu kila kukicha kwani mwanaume anatoka na pia anakaa na wenzake, walio wengi husimuliana mambo yanayowapagawisha wawapo faragha.

Uvaaji wako wa nguo za ndani unaweza kuwa sauti ya kumwamsha mwenzi wako usingizini na kuitikia hisia zako.

UCHAGUZI WA RANGI

Hili nalo ni msingi sana, wengi wanaweza kufaulu katika hatua ya namna gani ya kuvaa nguo zenye mvuto kwa mwenzi wake lakini wakashindwa kuelewa rangi tu inaweza kuhamasisha mwenzi wako au kumfanya asijisikie chochote.

Kama wewe ni mweusi unashauriwa kuvaa rangi nyeupe ili kumuweka ‘attention’ mwanaume pale unapopita mbele yake. Mkiwa chumbani kwenu, unaweza ukapita mbele yake kwa madaha ukionyesha kuwa unahitaji ukaribu wake.

Ukijidanganya na kutumia rangi nyeusi utaula wa chuya! Kama wewe ni mweupe, rangi zako wewe ni nyingi, ikiwemo nyeusi lakini haivutii sana. Epuka rangi hiyo, wewe cheza na nyeupe, pinki, nyekundu hata kijani bora iwe inawaka, itakusaidia kurudisha mawazo ya baba watoto nyumbani.

Hakikisha nguo hizo zinakuwa spesho na zenye mvuto, ambazo huwezi kuvaa nyakati za kawaida unapokwenda kazini, hizo ziwe kwa ajili ya mumeo tu, kwani kila akiona umemvalia vazi hilo anakumbuka wajibu wake.

Acha kuvaa kanga kila siku, kuwa mbunifu na umsogeze mumeo karibu, utayafurahia mapenzi kwa hakika. Kwanini usiwe mbunifu na kumvuta mume wako karibu yako? Wanawake wengi huishia kulalama kutopata ushirikiano wa kutosha kwa wenzi wao, lakini mwisho wa siku kumbe uwezo wa kuboresha ni wao wenyewe. Bila shaka somo limeeleweka vema. Nawatakieni wikiendi njema. Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano, ameandikia vitabu kama True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha SIRI ZA NDOA YENYE FURAHA kitakachotoka hivi karibuni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.